MRADI WA MAJI KIJIJI CHA UTWEVE WAANZA KUTOA HUDUMA MAKETE

 📌MWANDISHI WETU  

Mkurugenzi Mkuu wa RUWASA Mhandisi Clement KIVEGALO amefanya ziara na kujionea ujenzi wa Mradi wa maji wa Kijiji cha Utweve Wilayani Makete Mkoa wa Njombe ambao umeanza kutoa huduma kwa wananchi kabla ya kukamilika kwa asilimia mia moja.

Mradi huo uliofikia asilimia 85 za utekelezaji umeanza kutoa huduma kwa wananchi huku ukiwa katika hatua za mwisho za utekelezaji. 

Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso ametoa maagizo ya kisekta kuwa utekelezaji wa mradi wa maji uanze kwenye chanzo kuelekea kwenye matangi ya maji na mwisho kusogezwa kwa wananchi. Lengo la agizo hili la Mheshimiwa Aweso ni kuhakikisha wakati mradi unatekelezwa maeneo ya mwanzo wananchi waanze kupata huduma ya maji.

Mradi wa maji wa Utweve unatekelezwa kwa kupitia wataalamu wa ndani (force account) kwa gharama ya shilingi 304,867,046.98 na utakapokamilika utahudumia zaidi wananchi mia saba wa kijiji cha Utweve.

Kazi zilizofanyika kwenye Mradi huu ni Ujenzi wa mtego wa maji, njia kuu ya maji urefu wa Mita 5250, tangi moja la lita 50,000, njia za usambazaji mabomba urefu wa Mita 6900, ujenzi wa uzio eneo la tangi na mtego wa maji, ujenzi wa vituo 15 vya kuchotea maji na Jengo la CBWSO-JUWAMAVILE. 

Post a Comment

0 Comments