SERIKALI KUBORESHA HUDUMA ZA KIBINGWA MKOANI IRINGA

 


📌WAF- DOM

SERIKALI Kupitia Wizara ya afya inaelekea kukidhi kiu ya Wananchi wa Mkoa wa Iringa kwa kupeleka kusoma jumla ya madaktari 12 watakaotoa huduma katika fani mbalimbali katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Afya Mhe. Dkt. Godwin Mollel leo Novemba 8, 2021 katika kikao cha bunge, Jijini Dodoma wakati akijibu swali la Mhe. Nancy Hassan Nyalusi Mbunge wa viti maalumu. 

Amesema, Katika kuongeza idadi ya madaktari bingwa, Wizara imepeleka kusoma jumla ya madaktari kumi na mbili (12) kutoka Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Iringa ambao watasaidia kuboresha huduma kwa wananchi wa Mkoa huo.

Akifafanua hilo Dkt. Mollel amesema, madaktari hao ni pamoja na; madaktari wawili wanasomea kinywa, sikio na koo, madaktari bingwa wa mifupa wawili, daktari wa magonjwa ya dharura mmoja, madaktari bingwa wa Watoto wawili, madaktari bingwa wa magonjwa ya ndani wawili, daktari bingwa wa meno mmoja, daktari bingwa wa usingizi mmoja na daktari bingwa mbobezi wa masuala ya Watoto mmoja. 

Aidha, Dkt. Mollel amesema, hadi sasa Hospitali hiyo ina jumla ya madaktari bingwa kumi na moja 11, madaktari bingwa wa afya ya akina mama na uzazi wanne, madaktari bingwa wa upasuaji wawili, daktari bingwa wa magonjwa ya ndani mmoja, daktari bingwa wa Watoto wawili, daktari  bingwa wa macho mmoja  na daktari bingwa wa mionzi mmoja.


Post a Comment

0 Comments