TANZANIA KUKABILIWA NA MAGONJWA YA KUAMBUKIZA KWA ASILIMIA 95

 ðŸ“ŒRHODA SIMBA

TANZANIA inakabiliwa na magonjwa ya kuambukizwa kwa asilimia 95% kutokana na baadhi ya wahudumu wa afya na wagonjwa  kutopenda kutumia huduma za maabara hali  iliyisababisha wagonjwa wengi kutibiwa bila kupata uhakiki wa majibu kutoka maabara.

Takwimu hizo zimetolewa Jijini Dodoma na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dk.Seif Shekalage kwenye kikao na wataalmu wa Afya ambapo amesema tatizo hilo limepelekea matumizi yasiyo rasmi ya antibiotiki ambayo husababisha usugu wa vimelea kuongezeka mwaka hadi mwaka mfano 1993 matumizi yalikuwa asilimia 39%, mwaka 2002 asilimia 42%, 2014 asilimia 67.7% na 2017 hadi 2022 wastani wa asilimia 65%.

Matokeo ya tafiti iliyofanyika mwaka 2017 yalionesha kwamba asilimia 92% ya wagonjwa hupata matibabu yao katika maduka ya dawa na famasi na kati yao asilimia 92.3% hununua antibiotiki holela bila kutumia cheti cha dawa kilicho idhinishwa na daktari

Aidha amesema kuwa umihimu wa dawa za antibiotiki katika maisha inajidhihilisha wazi ikirejea na historia ya uvumbuzi wake, ambapo kati ya wagonjwa 100 waliougua nimonia au maambukizi ya vidonda wagonjwa 90 walikuwa wakifariki. 

Ambapo Uvumbuzi wa antibiotiki ya kwanza aina ya penicillin ulibadili hali na kupunguza vifo hadi kufikia vifo 10 kati ya wagonjwa 100, Matumizi mabaya ya dawa jamii ya penicillin yameshapelekea dawa iyo kujenga usugu kiasi kikubwa. 

Amesema Tanzania, kama ilivyo kwa nchi nyingine zinazoendelea, inakabiliwa na magonjwa ya kuambukizwa kwa asilimia 95%, kutokana na baadhi ya watumishi kutopenda kutumia huduma za maabara hali iliyosababisha wagonjwa wengi kutibiwa bila kupata uhakiki wa majibu kutoka maabara.

Usugu wa vimelea dhidi ya dawa unatuweka katika mashaka makubwa ya kupoteza nguvu kazi ya Taifa hili kwa kusababisha vifo kutokana na kuongezeka kwa magonjwa sugu yasiyotibika kwa kutumia dawa tulizonazo; kuongezeka kwa umaskini kutokana na kuugua kwa muda mrefu na kutumia dawa za ghali zaidi; na pia kuongezeka kwa vifo vya mifugo na uzalishaji hafifu wa chakula, na pia kuigharimu nchi mamilioni ya fedha ambazo zingeweza kutumika kuliletea Taifa letu maendeleo 

Naye Mfamasia Mkuu wa Serikali Daud Msasi akabainissha namna Serikali inavyochukua Hatua pale wanapopata taarifa ya changamoto za dawa.

Serikali inafanya nini kwenye hizi dawa ni sisi kama serikali tunafanya tafiti katika dawa mbalimbali ambazo zinafanyiwa tafiti na wanasayansi kutoka Chuo kikuu cha Muhimbili na kutoa taarifa na Serikali ikigundua kuwa kuna changamoto yoyote kwenye dawa tunakuwa na kazi ya kuhuwisha miongozo kila baada ya miaka 3 na tukipata taarifa ambazo ni nzuri zaidi hapo kati hata kabla ya miaka 3 kutimia tunatoa zile dawa kwa sababu zinakuwa hazimtibu mtu yeyote

Lengo la maadhimisho haya ni kusisitiza na kuongeza uelewa juu ya matumizi sahihi ya dawa hizi ili kupunguza matumizi yasiyostahili na hatimaye kuzuia ongezeko la usugu wa vimelea dhidi ya dawa, ambapo ujumbe wa mwaka huu unasema “Preventing Antimicrobial Resistance Together” yaani “Kwa pamoja tuzuie usugu wa vimelea dhidi ya dawa”, Jambo la kuzuia usugu ni letu sisi sote, hivyo kwa pamoja sekta zote (Afya, Mifugo,Uvuvi,Kilimo na Mazingira) tuungane katika kuhakikisha tunapunguza au kuzuia usugu wa vimelea dhidi ya dawa.

Kuanzia tarehe 18-24 Novemba ya kila mwaka duniani kote tunaadhimisha wiki ya kampeni ya dawa aina ya antimicrobials (World Antimicrobials Awareness Week).

 


 

 

 

Post a Comment

0 Comments