TCRA: TUMETOA LESENI ELFU 3,132 KATIKA MAKUNDI SITA


📌RHODA SIMBA

Mamlaka ya Mawasiliano nchini TCRA imetoa leseni 3,132 katika makundi aina 6 ikiwemo leseni ndogo za ufungaji, utengenezaji, uangizaji na usambazaji wa vifaa vya simu 2,161.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya mawasiliano nchini Dkt. Jabir Bakari wakati akizungumza na waandishi wa habari kuelezea mafanikio ya mamlaka hiyo kwa mwaka wa fedha 2022/2023 ya kudhibiti anga ya mawasiliano ya nchi kuanzia September hadi November Jijini Dodoma .
Aidha akibainisha Leseni hizo Dkt. Jabir amesema kwamba leseni hizo  ni pamoja na leseni za miundombinu ya mawasiliano 22, utumiaji wa miundombinu ya mtandao 10, matumizi ya huduma 107, huduma maudhui 741 television 61, mtandao 390 cable TV 65, Radio 218 sanjari na radio mtandao 7.

Kwa mujibu wa Dkt. Bakari ameendelea kuzitaja leseni hizo ni pamoja na Posta na usafirishaji wa vifurushi 91 tofauti na awali 120 huku akibainisha kwamba TCRA inasimamia shughuli za mawasiliano ya simu na intaneti kwa kuhakikisha zinatolewa kwa viwango vya kimataifa vilivyowekwa na EPOCA.

Aidha TCRA imesema kuwa inahakikisha mifumo ya usimamizi wa mawasiliano ya simu intaneti kwa serikali kuanzisha mfumo uitwao TTMS ambao husimamia na kuratibu mawasiliano ya simu yenye uwezo wa kubaini takwimu mbalimbali zinazopita katika mitandao ya mawasiliano kwa watoa huduma.

Akabainisha kwamba TCRA imejikita kuhakikisha maudhui yanayorushwa na vituo vya utangazaji nchini yanazingatia weledi maadili ya uandishi wa habari pia hayakiuki sheria na kanuni zinazosimamia sekta ya utangazaji.

Hata hivyo sekta ya mawasiliano ya simu nchini imeendelea kukua hadi kufikia Septemba 2022 kulikuwa na laini za simu 58.1 milioni ambazo zinajumuisha laini zinazotumiwa na watu na mashine kwa mashine huku akieleza mikoa inayoongoza ikiwa ni Dar es Salaam laini milion 9.756 Mwanza milion 3.700 Arusha milion 3.448 Mbeya milion 3.089 na Tabora milion 3.060.

Akielezea gharama za muunganisho wa simu kutoka mtandao mmoja kwenda mwingine zimekuwa zikipungua mwaka hadi mwaka 2015 zilikuwa TZS 30.58 na kwa sasa ni TZS 2.00 na kusaidia kupungua gharama za jumla za upigaji simu na kuondoa ulazima wa wateja kuwa na simu zaidi ya moja. 

Kwa muktadha huo licha ya mafanikio hayo sekta hiyo inakumbana na changamoto kadhaa ikiwemo ya uharibifu wa miundombinu ya mawasiliano, utoaji wa huduma za mawasiliano kwa wote maeneo ambayo hayajafikiwa mahitaji makubwa ya bendi za masafa usalama wa mtandao na uhalifu mtandao kudhibiti maudhui ya mtandao na ubora wa huduma za mawasiliano.

Naye Msemaji Mkuu wa Serikali  Gerson Msigwa amesema serikali imetenga fedha zaidi ya shilingi bilioni 600 kwaajili ya mkongo wa taifa na kwa uwekezaji uliofanywa na serikali kupitia TCRA na uimara wa vyombo vya dola hakuna mtu anaeweza kufanya uhalifu mtandaoni akabaki salama.

Mamlaka ya mawasiliano Tanzania (TCRA), ni Taasisi ya serikali yenye jukumu la kusimamia sekta ya mawasiliano nchini ikiwa na majukumu ya kuhimiza ushindani bora na uchumi wenye tija, kulinda haki na maslahi ya watumiaji, kuimarisha elimu kwa umma na kuhamasisha upatikanaji wa huduma za mawasiliano kwa watumiaji wote ukijumuisha watumiaji wenye kipato kidogo, walioko vijijini na watumiaji ambao wako katika maeneo yasiyokuwa na mvuto wa kibiashara.

 

Post a Comment

0 Comments