WANANCHI WAASWA KUWAPA USHIRIKIANO WATOA HUDUMA YA CHANJO YA POLIO AWAMU YA NNE

 ðŸ“ŒRHODA SIMBA 

KATIKA kupambana na Ugonjwa wa Polio  Serikali imesema kuwa imeweka mikakati ya kukabiliana na Ugonjwa huo  ikiwa ni miongoni mwa magonjwa hatarishi zaidi kwa watoto na inabainishwa kuwa  virusi vya polio huvamia mfumo wa neva na madhara yake husababisha kupooza au hata kifo.

Kauli hiyo imetolewa leo na Afisa Program Chanjo  Lotalis Gadau  wakati wa utoaji semina elekezi kwa wanahabari jjini Dodoma iliyolenga kutoa elimu kuelekea katika kampeni ya polio.

Aidha  amesema kampeni hiyo itakuwa ni nyumba kwa nyumba kwa utoaji wa chanjo za matone ya Polio lengo likiwa ni kuwafikia watoto kuanzia umri chini ya miaka mitano ambapo licha ya kuwa na  timu za wachanjaji pia  kutakuwepo na waangalizi wa kujitegemea katika kila Mkoa nchini ili kukamilisha zoezi hilo.

Ametaja njia za maambukizi ya ugonjwa huo sambamba na dalili ikiwa ni pamoja na homa, uchovu, maumivu, ya kichwa, kutapika, kukakamaa shingo na maumivu ya Viungo.

Ugonjwa huu huambukizwa kwa kuingia mwilini kwa njia ya mdomo, kunywa Maji,au chakula ambacho kimechafuliwa na kinyesi kutoka kwa mtu aliyeambukizwa virusi hivyo na virusi huongezeka ndani ya utumbo na hutolewa na mtu aliyeambukizwa kwenye kinyesi, ambacho kinaweza kupitisha virusi kwa wengine

Aidha ameeleza hali ilivyo kwa sasa juu ya ugonjwa wa Polio katika maeneo mbalimbali ndani ya Bara la Afrika.

Zambia tayari kuna kisa kimoja, wenyewe wanajiandaa na awamu ya Tatu, na kwetu Tanzania tunamshukuru mungu bado kisa ni kile kile hatujapata kingine, lakini bado hakijalemaa, bado tunaendelea na ufuatiliaji kwa kuchukua Sampuli kuhakikisha kwamba tunapeleka maabara mwisho wa siku watoto wetu wawe salama.DRC CONGO bado kuna vimlipuko vya hapa na pale lakini ambao tulienda nao sambamba tokea tunaanza mwanzo ni Malawi, Msumbiji, Zimababwe na Zambia

Pia ameeleza mikakati inayotumika katika kuhakikisha wanatokomeza ugonjwa huo hapa nchini ikiwa ni pamoja na kufanya kampeni za kutoa elimu itakayoambatana na utoaji wa Chanjo.

Tunachojitahidi ni kuonesha kwamba tunaimarisha utoaji wa chanjo za kila siku kuhakikisha kwamba watoto wetu wanakamilisha Ratiba zao za chanjo ili endapo hata Kirusi kikija kikimkuta mtoto ameshapata kinga kamili kinakuwa hakina nafasi na kwa awamu hii tunalenga kuwafikia watoto wapatao Millioni 14 laki sita na Tisini, Mia tano Tisini na Saba kwa awamu hii ya nne

Awali akifunga mafunzo hayo Mratibu wa Chanjo Mkoa wa Dodoma  Dkt. Francis Bujiku amewataka wananchi kutoa ushirikiano pindi wanapowaona watoa huduma kwa kuwatoa watoto ili wapate Chanjo ya Polio ya matone ili  kuongeza kinga dhidi ya ugonjwa wa Polia ambao ni mkali na una madhara kwa watoto .



 

Post a Comment

0 Comments