MIRADI YA MAJI ILIYOTEKELEZWA KWA FEDHA ZA MAPAMBANO DHIDI YA UVIKO 19 YALETA MANUFAA KILOLO

📌MWANDISHI WETU

Mradi wa Maji wa Nyamlenge uliotekelezwa kwa fedha za mapambano dhidi ya ugonjwa wa Uviko 19 umeleta manufaa kwa wakazi wapatao 1675 wa kijiji cha Neghabihi Wilayani Kilolo Mkoa wa Iringa.

Akiendelea na ziara yake Mkoani Iringa Mkurugenzi Mkuu wa RUWASA Mhandisi Clement KIVEGALO amefurahishwa na utekelezaji wa mradi huo uliofanywa na Mkandarasi kampuni ya M/S GNMS CONTRACTORS CO.  Ltd kwa gharama ya shilingi 299,098,050.

Mradi ulihusisha ujenzi wa tangi la lita 150,000, uchimbaji wa mtaro na ufukiaji wa bomba urefu wa kilomita 10.24, ujenzi wa vituo 11 vya kuchotea maji kwa jamii pamoja na ujenzi wa nyumba ya pampu.

Mradi kwa sasa umekamilika na upo kwenye muda wa matazamio kwa kipindi cha mwaka mmoja.




Post a Comment

0 Comments