TRA YAWAFIKISHA MAHAKAMANI WASIO DAI RISITI ZA EFDS

 ðŸ“ŒRHODA SIMBA 

MAMLAKA ya Mapato Tanzania TRA imewafikisha mahakamani watuhumiwa wa makosa ya kutodai risiti za Kielektroniki baada ya manunuzi ya bidhaa mbalimbali waliyofanya huku ikitoa wito kwa wafanyabiashara kote nchini kuhakikisha wanatoa risiti kwa kila mauzo kwa kuwa ni takwa la Kisheria.

Makosa ya watuhumiwa hao ni pamoja na wanunuzi hao kutotoa ushirikiano kwa maafisa wa TRA utakaowawezesha kuwatambua wafanyabiashara wanaouza bila kutoa risisti, kutoa taarifa za uongo pamoja na baadhi ya wafanyabiashara kutowasilisha katika mamlaka taarifa za hesabu za Mwaka.

Shauri la Jinai namba 171 mwaka 2022 limetajwa kwa mara ya kwanza katika mahakama ya wilaya ya Dodoma chini Kifungu cha 86, kifungu kidogo cha 4 cha sheria ya usimamizi wa kodi namba 10 ya mwaka 2015 kwa kosa la kutodai risiti ya EFD.

Kuhusu kosa la pili la kutotoa ushirikiano watuhumiwa wanashtakiwa kwa mujibu wa kifungu 85, kifungu kidogo 3 (h) cha sheria ya Utawala wa Kodi na Usimamizi wa Kodi namba 10 ya mwaka 2015.

 

Post a Comment

0 Comments