PSPTB KUENDELEA KUCHUKUA HATUA MADHAIFU KWA WAKUU WA VITENGO VYA UNUNUZI NA UGAVI

 ðŸ“ŒRHODA SIMBA

MKURUGENZI Mtendaji wa Bodi ya Wataalam wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB), Godfred Mbanyi amesema  kuwa Bodi hiyo imekuwa ikichukua hatua katika madhaifu ambayo yanaweza kuleta hasara kwa serikali na kuathiri Miradi mikubwa kwa wakuu wa vitengo vya Ununuzi na Ugavi.

Akizungumza jijini hapa leo Januari 19, 2023 wakati wa kutoa taarifa ya matokeo ya mitihani ya 25 ya Bodi hiyo Mkurugenzi huyo amesema wanachosisitiza ni somo la hebabu na ni dhana ambayo imejengwa tangu chini kuwa somo hilo ni gumu kitu ambacho sio sahihi hesabu inafaulika.

Mkurugenzi huyo ameeleza kuwa mtaalamu wa manunuzi ni vizuri ajue hesabu ambayo itamsaidia kujiamini na kuandika ripoti katika shughuli zake na kwamba Ununuzi na Ugavi unaakisi zaidi katika uelewa wa manunuzi, uelewa wa dhana nzima mtambuka katika ule mzunguko wa shughuli za kimanunuzi kwa kuwa anatakiwa kupiga hesabu katika uwiano mbalimbali.

Tunachukua hatua pale tunaona kuna madhaifu ambayo yanaweza kuleta hasara kwa serikali na pia inaweza kuathiri utoaji huduma kwa watu hasa katika miradi mikubwa

Mbanyi.

Ameongeza kuwa kumekuwa na mamalamiko kwa baadhi ya wanunuzi na kwamba wao kama Bodi mwaka wa fedha uliopita waliamuru Wakuu wa vitengo 20 kuondolewa kwenye nafasi zao baada ya kutathimini taarifa ya matumizi ya Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA), na Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).

Mkurugenzi huyo amesema kuwa tayari wameshatuma barua 73 kuwaeleza makosa waliyoyafanya, udhaifu na makosa yaliyoonekana kwenye manunuzi na wanunuzi 68 kupeleka utetezi wao katika Ofisi ya Bodi.

Akizungumzia matokeo hayo amesema jumla ya watahiniwa 1,216 walisajiliwa kufanya mitihani ambapo watahiniwa 1,135 sawa na asilimia 93.3 walifanya mitihani hiyo na kwamba kumekuwa na ongezeko la watahiniwa 1,031, ikilinganishwa na msimu uliopita.

Kati ya watahiniwa waliofanya mitihani hiyo watahiniwa 452 ni wapya na waliobaki 683 ni watahiniwa waliokuwa wanarudia baadhi ya masomo," amesema Mkurugenzi huyo.

Mbanyi ameeleza kuwa jumla ya watahiniwa 613 sawa na asilimia 54.0 wamefaulu mitihani yao ambapo watahiniwa 474 sawa na asilimia 41.8 watarudia baadhi ya masomo kuanzia moja hadi masomo matatu kutegemeana na idadi ya masomo aliyofeli na watahiniwa 48 sawa na asilimia 4.2 wamefeli masomo yote katika ngazi mbalimbali.

Katika masomo 34 waliyopimwa watahiniwa, masomo 18 yalifanywa vizuri, masomo 10 yalifanywa kwa wastani na matokeo ya masomo 6 yalikuwa mabaya kwa maana ya kuwa chini ya wastani. Huku watahiniwa watatu wakiibuka kama watahiniwa bora katika ngazi za mitihani za Professional I, iii na CPSP.

Post a Comment

0 Comments