SERIKALI IMEWEKA MIFUMO MAKINI JUU YA BIASHARA MTANDAO

 ðŸ“ŒJASMINE SHAMWEPU

WAZIRI wa Habari , Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Nape Nnauye amesema kuwa ili kupanua wigo wa biashara mtandao Serikali imeweka mifumo ya Sera, Sheria na usimamizi wenye umakini juu ya biashara mtandao na kuendeleza uwekezaji wake kwa viwango vya juu.

Pia Nchi ya Tanzania imejipanga kuwa kitovu cha biashara mtandao inayovuka mikapa barani Afrika kwa kupanua wigo wa kasi ya ukuaji wa Teknolojia na kuwa sekta tegemezi katika kukuza uchumi.

Waziri Nnauye ameyasema hayo leo jijini Dodoma wakati akizungumza kwenye maadhimisho ya siku ya Posta Afrika na kueleza kuwa umuhimu wa Posta unawezesha umahiri wa biashara kidigitali.

Waziri huyo pia amesema kwa kuwa Serikali inatambua kuwa biashara mtandao ni kipaumbele kwa nchi za Afrika itawekeza zaidi katika usalama, amani, urahisi na ufanisi mtandaoni ili kuchochoea mageuzi ya Afrika kidigitali.

Umuhimu wa Posta, sisi kama Serikali tumejipanga kukamilisha ujenzi jengo la Posta Afrika lenye makao yake makuu Jijini Arusha, hivyo niwaombe nchi wanachama wa Posta Afrika kutekeleza kwa wakati maazimio yaliyowekwa

Katika kutekeleza yote hayo, Mkurugenzi wa Mamlaka ya mawasiliano Tanzania (TCRA) Jabiri Bakari Kuwe amesema mamlaka hiyo itaendelea kuweka mazingira ya kuvutia kibiashara ili kukabiliana na soko la kimataifa.

Amesema wao kama wadau wa Posta wamejipanga kuongeza wigo wa Teknolojia kuendana na viwango vya kimataifa ikiwa ni pamoja na kushughulikia changamoto na vikwazo vilivyopo mipakani.

Amesema upatikanaji wa bidhaa na kuwezesha wananchi kununua bidhaa hadi mlaji, lengo letu kubwa ni kuongeza mnyororo wa usambazaji bidhaa kidigitali.



 

 

Post a Comment

0 Comments