SERIKALI YAUNDA KAMATI KUTATHIMINI UCHUMI WA VYOMBO VYA HABARI

 


📌RHODA SIMBA

SERIKALI kupitia Wizara ya Habari ,Mawasiliano na Teknolojia ya Habari  imeunda kamati kwa ajili ya kutathimini vyombo vya habari kiuchumi na kiutendaji.

Akiongea na waandishiwa habari  leo,Januari 24,2023 ,Waziri wa Wizara hiyo Nape Nnauye    amesema kuwa hayo ni  kutokana na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassani kutoridhishwa na uchumi wa vyombo vya habari na waandishi wa habari ambapo ameagiza wizara kuona namna ya kushughulikia  jambo hilo na kulifanyia utatuzi.

Nape amesema kuwa kutokana na agizo la Rais,Wizara hiyo imeunda kamati ya watu nane ikiongozwa na Tido Mhando ambaye ni mwenyekiti,Gregson Msigwa Katibu,Dk.Rosse Rubeni Mjumbe,Joyce Mhavile, Mjumbe,Sebastian Maganga, Mjumbe,Bakari Machumu,Mjumbe,Kenneth Sembeya Mjumbe,Jackiline Owiso Mjumbe ambapo leo amemuongeza mjumbe mwingine ambaye ni mwandishi wa habari ,Richard Mwaikenda. 

Nape amesema kuwa kamati hiyo inatakiwa kuwa imekamilisha kazi hiyo ndani ya miezi mitatu sawa na siku tisini.

Amesema kuwa kazi kubwa ya kamati hiyo ni pamoja na kamati kufanya tathimini ya hali ya uchumi kwa vyombo vya habari kielimu na kiutendaji ,hali ya waandishi wa habari  na vyombo vya habari,kuhusu ajira,vipato,mikataba na wawakilishi waliopo mikoani.

Aidha kamati hiyo itatakiwa kutoa taarifa kwa jinsi utekelezaji wa  mikataba na ajira vinavyo heshimiwa sambamba na pia kutafuta changamoto inayosababisha changamoto ya kiuchumi na changamoto ya kutekeleza kupitia vyombo vya habari serikali na wadau.

Aidha Nape amesema kuwa kazi ya kutafuta maoni ni ya watu wote hivyo watanzania pamoja na wanahabari wanatakiwa kutoa ushirikiano ikiwa ni pamoja na kutoa maoni kwa njia ya Mtandao na mchakato wa mabadiliko ya sheria ya huduma ya vyombo vya habari umefikia pazuri  na tayari umeshapelekwa kwa mwanasheria mkuu wa Serikali.

Vilevile amesema kuwa kutokana na kuwepo kwa matapeli ambao wanatumia laini za simu vibaya  ifikapo mwenzi ifikapo Februari 13 mwaka huu saa kumi jioni laini zote ambazo hazijahakikiwa zitazimwa.

Zaidi ya laini za simu milioni 60 zimesajiliwa na zaidi ya milioni 58 zimehakikiwa,zaidi ya milioni 2 hazijahakikiwa hivyo kutokana hali hiyo zitafungiwa na hazitakuwepo hewani kabisa,

Wito wangu kwa watanzania ni wakati mzuri sasa wa kuhakikisha kila mwenye laini ya simu na hata kama kuna mtu ambaye alisajiliwa laini yake na ndugu yake kwa kutokana na changamoto ya NIDA ni wakati mzuri sasa wa kufanya uhakiki na pindi line zikifungiwa hazitafunguliwa tena na hakuna muda tena utakao ongezwa

Nape.

 

Post a Comment

0 Comments