WIZARA YA KILIMO YAWANOA WAHARIRI KUHUSU TATIZO LA SUMU KUVU.

 ðŸ“ŒRHODA SIMBA

ILI kuelimisha jamii kuhusu udhibiti wa tatizo la sumu kuvu Wizara ya Kilimo kupitia mradi wake wake wa (TANPAC) imewakutanisha wahariri wa vyombo mbalimbali kwa ajili ya kuwapatia semina yenye lengo la kwenda kutoa elimu katika jamii.

Akiongea katika semina hiyo, Mratibu wa Mradi wa kudhibiti Sumukuvu Clepin Josephat amesema tatizo la sumukuvu hapa nchini Tanzania limeanza 2016 katika Mkoa wa Dodoma.

Amesema Malengo ya mradi huo pamoja na mambo mengine ni kuimarisha usalama wa chakula hapa nchini, kuimarisha uchumi wa nchi kupitia mauzo ya chakula nje ya nchi pamoja na kuimarisha Afya ya jamii.

Aidha Clepin amesema ili kufikia malengo hayo mradi huo unajenga miundombinu ya msingi katika kudhibiti Sumukuvu lakini pia umelenga kuimarisha taasisi za udhibiti na utafiti ili udhibiti wa sumukuvu uwe endelevu.

Kwa upande wake Mhadhiri kutoka Chuo Kikuu Huria Dkt. Happy Magoha amesema elimu kuhusu usalama wa chakula inatakiwa kutolewa mara kwa mara,ili kuepuka mazao kupata Sumu kuvu ikiwemo kuepusha madhara kwa jamii.

Amesema elimu hiyo inatakiwa kutolewa kwa jamii mara kwa mara ili kuhakikisha jamii inatambua umuhimu wa kuhifadhi vizuri mazao ili yasipate Sumukuvu ambayo ina madhara kwao.

 

Post a Comment

0 Comments