ACHENI KULAGHAI WAKULIMA; MKURUGENZI WRRB

 ðŸ“ŒRHODA SIMBA

KUFUATIA kuwepo kwa vitendo vya ulanguzi usio halali wa mazao kwa wakulima hapa nchini Bodi ya Usimamizi wa Stakabadhi za Ghala (WRRB) imetoa wito kwa walanguzi wa mazao kuacha kuwalagai wakulima kwa lengo la kujinufaisha. 

Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi hiyo Asangye Bangu wakati akielezea utekelezaji wa shughuli mbalimbali za bodi hiyo kwa  waandishi wa habari leo Februari 15,2023 jijini Dodoma.

Amesema kuwa kumekuwa na wimbi la watu wanakwenda mashambani kwa wakulima na kuwadalalia mazao na kununua kwa bei ya chini kitu ambacho kinaendelea kudidimiza maendeleo ya wakulima.

Natoa wito kwa madalali waache kuwarubuni wakulima wawaache wajiunge katika Mfumo wa Stakabadhi ghalani ili waweze kuuza mazao yao kwa bei ya ushindani iliyopo sokoni kwa kuendelea kuuza mazao shambani inaendelea kuwadidimiza wakulima kwa sababu madalali wengi wananunua mazao kwa bei ya chini tofauti kabisa na bei iliyopo kwenye mfumo

Bangu

Bangu amesema mafanikio yaliyopatikana baada ya kuanzishwa kwa Mfumo wa Stakabadhi za Ghalani pamoja na ongezeko la bei za mazao, mapato ya mkulima na mapato ya Serikali kwa wastani wa asilimia 200% kutokana na urasimishaji, ongezeko la uzalishaji wa mazao kwa wastani wa asilimia 12% kwa mwaka, kichecheo cha ubora wa mazao yanayofikishwa sokoni,

Ametaja mafanikio mengine ni upatikanaji wa takwimu sahihi za mazao yanayopita kwenye Mfumo wa Stakabadhi za Ghala, ongezeko la mapato ya uhakika kwa Serikali Kuu na Serikali Mitaa na kukuza huduma za fedha vijijini, kufanikisha uanzishaji wa Soko la Bidhaa Tanzania.

Aidha, Mkurugenzi huyo amesema kuwa tangu kuanzishwa kwa Mfumo 2007/08 hadi 2020/21 ukuaji wa uzalishaji umekuwa ukiongezeka kwa wastani wa 12% kwa mwaka ikilinganishwa na ukuaji wa 2% kwa mwaka kabla ya kuanzishwa kwa Mfumo wa Stakabadhi za Ghalani

Kwa mfano katika zao la Korosho mara baada ya kuanzishwa kwa Mfumo palikuwa na ongezeko la asilimia 164% la bei kutoka Ths 350.00 msimu wa 2006/07 hadi kufikia Tsh 925.00 msimu wa 2007/08 mwaka wa kuanza wa Mfumo; katika miaka minane tokea kuanzishwa kwa Mfumo 2007/08 hadi 2014/15 wastani wa ongezeko la bei kwa mwaka ulikuwa 25% kulinganisha na ongezeko la bei miaka minane kabla ya kuanzishwa kwa Mfumo la 12% kwa mwaka kaunzia mwaka 1998/99 hadi 2006/07

 Bangu

 

Post a Comment

0 Comments