AWESO AWATAKA WAHANDISI KUTATUA CHANGAMOTO YA MAJI KWA WANANCHI

 ðŸ“ŒJASMINE SHAMWEPU

WAZIRI wa Maji Mheshimiwa Jumaa Aweso amewataka Wahandisi wa Maji kwenda kufanya kazi kwa bidii ili kutatua changamoto ya Maji inayowakabili wananchi hapa nchini.

Aweso ameyasema hayo leo Jijini Dodoma alipokuwa kwenye Mkutano Mkuu wa mwaka wa Sekta ya Maji uliofanyika katika Ukumbi wa Halmashauri ya Jiji Mtumba.

Amesema Wizara ya Maji haijengwi na Aweso bali inajengwa na watu wote hivyo wanapaswa kushirikiana ili kuleta maendeleo katika Sekta ya Maji.

Moja ya changamoto kubwa ya watumishi wangu kwa dhati ya moyo katika kipindi nilipoingia kwenye Wizara yetu ya Maji hampendani, yupo tayari mtu kumuona mwenzake anaumia bila kumsaidia, pendaneni ndugu zangu, kazi zetu zina changamoto nyingi mno

 Aweso.

Waziri huyo amesema Mfuko wa Maji lazima ulete matokeo chanya juu ka kuanzishwa kwake na hivi karibuni unakwenda kukopesha mikopo katika shughuli mbalimbali.

Aidha, Aweso ameitaka mamlaka ya Udhibiti Nishati na Maji (@ewura_tz) kuhakikisha inazibana Mamlaka za Maji zilizopo katika Sekta hiyo.

 

Post a Comment

0 Comments