BARAZA LA TAIFA LA UJENZI LIMETAJA VIPAUMBELE MWAKA WA FEDHA 2023

 ðŸ“ŒRHODA SIMBA

BARAZA la Taifa la Ujenzi  limesema,moja ya jukumu wanalopaswa kulifanya katika mwaka wa fedha wa 2022/23 ni pamoja na kukamilisha muongozo wa gharama za ujenzi wa barabara nchini kwa kuandaa gharama za msingi za mkandarasi kwa kila mkoa Tanzania bara.

Hayo yamesemwa jijini Dodoma na  Mtendaji Mkuu  wa baraza Hilo Dkt Matiko Mtani wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu utekelezaji wa majukumu yao  ambapo amesema pia baraza litaandaa mapendekezo ya kuboresha sheria na miongozo inayosimamia ujenzi wa majengo nchini.

Aidha  amesema baraza hilo litaandaa viwango msawazo vya majengo ya serikali, kutoa mafunzo ya kujenga uwezo kwa wadau wa sekta ya ujenzi nchini na kutoa fahirisi za bei za vifaa, mitambo na ujira katika shughuli za ujenzi kwa kila mwezi ili kuonyesha mabadiliko ya bei ya vifaa vya ujenzi.

Baraza hili vile vile lina jukumu la kusimamia utatuzi wa migogoro inayotokea katika miradi ya ujenzi, kutoa ushauri wa kiufundi kwa wadau mbalimbali wa sekta ya ujenzi , kuanza maandalizi ya kuwa na wiki ya ujenzi nchini na kukamilisha maandalizi ya kanuni za utekelezaji wa sheria ya Baraza hilo.

Dkt.Matiko

Akizungumzia mwelekeo wa taasisi hiyo Dkt.Matiko amesema, kufuatilia utekelezaji wa sera ya ujenzi nchini, kuandaa na kutekeleza mpango mkakati wa maendeleo ya sekta ya ujenzi na kutoa miongozo mbalimbali ya kitaalam ya maeneo mbalimbali ya ujenzi.

Kwa mujibu wa Mtendaji Mkuu huyo pia mwelekeo ni kuanzisha kituo cha taarifa za sekta ya ujenzi ambacho kitakuwa muhimu sana kwa wadau kupata taarifa muhimu za sekta ya ujenzi ikiwa ni pamoja na kuendeleza tafiti na Teknolojia.

 

 

Post a Comment

0 Comments