BILIONI 54.2 ZATUMIKA KUTEKELEZA MIRADI UJENZI WA NYUMBA ZA WATUMISHI WA UMMA.

 ðŸ“ŒRHODA SIMBA 

KATIKA kipindi cha miezi 18 Serikali imetoa kiasi cha  shilingi bilioni 54.2 kwa wakala wa majengo Tanzania (TBA) kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ikiwemo ujenzi wa nyumba za makazi na viongozi.

Mtendaji Mkuu wa Wakala huo Daudi Kondoro, amebainisha hayo Leo Februari 14, 2023, jijini Dodoma wakati akitoa taarifa ya utekelezaji wa shughuli mbalimbali za wakala huo kwa waandishi wa habari.

Amesema kiasi hicho cha fedha kimetumika katika ujenzi wa miradi mbalimbali ya ujenzi wa nyumba za makazi kwa watumishi wa Umma katika mikoa mbalimbali.

 

Post a Comment

0 Comments