eGA YASAIDIA KUDHIBITI UPOTEVU WA MAPATO.

 ðŸ“ŒRHODA SIMBA

MKURUGENZI Mkuu wa Mamlaka ya Serikali Mtandao (eGA) Mhandisi Benedict Ndomba amesema mfumo wa kielektroniki wa Gepg tangu kuanzishwa umesaidia kwa kiasi kikubwa kudhibiti upotevu wa mapato hapa nchini.

Mhandisi Ndomba, ameyasema hayo leo Februari 23 jijini Dodoma wakati akitoa taarifa kwa vyombo vya habari kuhusu utekelezaji wa shughuli mbalimbali za Mamlaka hiyo ambapo amesema tangu kuanzishwa kwa mfumo huo umesaidia kudhibiti mianya ya ukwepaji wa malipo mbalimbali ya Serikali.

Gepg imesaidia sana ukusanyaji wa mapato ya serikali kuona na kuwa na uoni wa mapato yake na sasa hivi mwenye mamlaka ya kuona anaweza kuona kuanzia asubuhi imekusanya shilingi ngapi na Taasisi fulani imekusanya shilingi ngapi na jana imekusanya bei gani hizi zote ni taarifa ambazo hapo awali hazikuwepo

Kwahiyo naweza kusema kwamba hiyo ni faida ya kwanza imeleta uoni mkubwa kwa Serikali, na pili ni kupata takwimu za makusanyo na huduma gani zinakusanya na zinailetea hela Serikali kiasi gani, hizi takwimu zote unazipata mtandaoni ukwepaji wa malipo huwezi kukwepa ukichukua namba ya malipo (control number) haitoki kwenye ile taasisi inatoka kwenye Gepg

 Mhandisi Ndomba

Aidha Mhandisi Ndomba amebainisha maeneo sita ya kipaumbele kwa mwaka wa fedha 2022/2023 ambapo amesema kama mamlaka itaendelea kusimamia sheria kanuni viwango na miongozo ya Serikali.

Tunaendelea kusimamia miongozo ya Serikali ikiwa ni pamoja na kukagua miradi na mifumo ya TEHAMA ya kimkakati kisekta na kitaasisi, kimkakati lakini pia inashauri maeneo ya kuboresha na kufatilia utekelezaji wa ushauri huo, kupitia na kutathimini hali ya usalama wa mifumo na miundo mbinu ya Serikali Mtandao na kushauri Taasisi za umma katika maeneo ya kuboresha.

Mamlaka ya Serikali Mtandao ni Taasisi ya Umma ya utoaji wa huduma kwa wananchi yenye Lengo la kuongeza ufanisi wa utendaji kazi katika Taasisi za Umma pamoja na kuboresha utoaji wa huduma kwa Umma ili huduma hizo zipatikane kwa urahisi, haraka na kwa gharama nafuu kupitia TEHAMA.

 

 

 

Post a Comment

0 Comments