IRUWASA KUJENGA MTO MTITU ILI KUKABILIANA NA MABADILIKO YA TABIA YA NCHI

 📌RAHMA HAJIA & GETRUDE VANGAYENA

MKURUGENZI Mtendaji wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Iringa (IRUWASA)  Mhandisi David Palangyo ameeleza hatua ambazo  mamlaka  imechukua ili kukabiliana na changamoto ya mabadiliko ya tabia ya nchi ikiwemo  kuunda vikundi vidogo vidogo ambavyo vinajihusisha na ufugaji wa nyuki pamoja na kupanda miti kando ya mto Ruaha.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma   Mkurugenzi huyo ameeleza utekelezaji wa majukumu ya mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira Iringa (IRUWASA) amesema kuwa mamlaka hiyo imeunda vikundi vya kujishughulisha na ufugaji wa nyuki ambapo nyuki hao husaidia kupambana na maadui na vikundi vingine vinajihusisha na upandaji wa miti kandokando  ya mto Ruaha ambapo itasaidia kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi.

Amesema kuwa mamlaka hiyo imeweza  kuwafikishia wananchi  huduma ya maji safi na salama kwa asilimia 97 kwa wakazi wa manispaa ya Iringa na inatoa huduma ndani ya masaa 23 kwa siku na hivyo basi imeweza kutimiza adhma ya serekali ya kumtua mama ndoo  kichwani.

Tumeweza kuvuka sera ya maji na ilani ya Chama Cha mapinduzi kwa kutoa huduma ya maji kwa asilimia 97 na tumeweza kumtua mama ndoo kichwani.

Hata hivyo amesema kuwa mamlaka hiyo imekuwa na mafanikio ya kitehama ambapo ni pamoja na kufunga mita za kisasa ambazo ni  mita za malipo ya awali (pre paid) ambazo zimeweza kuwafikia wanachi takribani 6700  kwa manispaa ya Iringa na taasisi za kiserekali.

Pia mamlaka hiyo imeandaa mipango mikakati ambayo itaweza kukabiliana na changamoto zinazoikabili ikiwemo ujenzi wa chanzo kingine cha Mto Mtitu katika manispaa ya Iringa ili kuongeza upatikanaji wa maji.

 

Post a Comment

0 Comments