MKURUGENZI MTENDAJI UTPC ATEMBELEA OFISI ZA KLABU DODOMA

Mkurugenzi Mtendaji Keneth Simbaya akisaini kitabu cha wageni leo katika ofisi za Klabu Dodoma
 
📌 FRED ALFRED

MKURUGENZI Mtendaji wa Muungano wa Vilabu vya Wandishi wa Habari Tanzania (UTPC) Kenneth Simbaya  leo Februari 11 ametembelea Ofisi za Klabu ya Wandishi wa Habari Mkoa wa Dodoma (CPC).

Pamoja na mambo mengine ameupongeza uongozi wa CPC huku akisisitiza njia bora za utatuzi wa migogoro.

Aidha amesema UTPC itaendelea kutoa mafunzo kwa waratibu wa vilabu  ili wawe na uwezo mkubwa wa utendaji kazi.

Nashuru leo nimekuja kuwatembelea sio ziara na haijawa rasmi sana lakini nimeona tukutane tubadilishane mawazo na nimefurahi kuona mnaendelea vizuri, na sisi UTPC tunahidi kuendelea kutoa mafunzo kwa waratibu ili wawe uwezo wa kujitosheleza itasaidia kujenga uwezo wa klabu kujitegemea
Mkurugenzi akisisitiza jambo wakati wa ziara hiyo leo ofisi za Klabu Dodoma

Mkurugenzi ikisalimiana na baadhi ya wanachama waliokuwepo ofisini leo wakiendelea na majukumu yao


Post a Comment

0 Comments