MSIGWA AWAPA TOMA JUKUMU LA KUHAKIKISHA HABARI ZA MTANDAONI ZINAKUWA NA WELEDI

 ðŸ“ŒASHA MWAKYONDE

MSEMAJI Mkuu wa Serikali na Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Habari Maelezo Gerson Msigwa amewataka waandishi wa habari mtandaoni kuzingatia uweledi  wa taaluma yao ikiwa ni pamoja na kutotumika na watu, makundi yenye nia mbaya kwa Taifa.

Pia Serekali imewataka wadau wa masuala ya habari na wamiliki wa vyombo vya habari kuzingatia weledi katika utendaji kazi wao hasa katika kipindi hiki cha Mapinduzi ya teknolojia na maudhui yanazingatiwa kuendana na taaluma hiyo.

Ameyasema hayo leo Februari 10 jijini Dodoma, wakati akizindua Taasisi ya Waandishi wa Habari za Mtandaoni (Tanzania Online Media Alliance -TOMA), Msingwa ameeleza kuwa ili kujitofautisha  na wanaotaka kuwatumia waaandishi  kwa maslahi  yao binafisi ni vema kulinda taaluma ya Habari.

Msingwa amesema Serikali inaona na kutambua juhudi za vyombo vya habari hali inayosababisha kutoa uhuru wa kutosha kwa kila mmoja kuanzisha na kumiliki chombo cha habari

Ameongeza kuwa kutokana na Teknolojia kukua Tasnia ya Habari imekuwa nguzo kubwa kwa sekta ya habari nchini huku akitoa angalizo kwa  kadri zinavyoongezeka inaonekana weledi wake unapungua .

Aidha amewataka TOMA kuhakikisha waandishi wa habari mtandaoni wanakuwa na uelewa mkubwa juu ya machapisho wanayotuma mtandaoni kwa kuwa imekuwa tegemeo kama chanzo kikuu cha habari.

Hafla hiyo imeandaliwa na Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Arusha (APC) ambao ndio waanzilishi wa Mtandao huu na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wa Habari nchini pamoja na wadau wa maendeleo ambao ni USAID, Freedom House, TAWLA, LHRC, JOWUTA , Wanachama waazilishi wa TOMA pamoja na wawakilishi mbalimbali kutoka katika Vilabu vya Waandishi wa Habari Tanzania 

Post a Comment

0 Comments