MUSWAADA SHERIA YA HUDUMA ZA HABARI KUPELEKWA BUNGENI APRILI

 ðŸ“ŒRHODA SIMBA

MSEMAJI Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa Msigwa amesema kuwa Serikali ilikusudia kupeleka muswaada wa Sheria ya Huduma ya Habari kwenye mkutano wa 10 katika Bunge ambalo linaendelea ili uweze kujadiliwa lakini kutokana na muda kuwa mdogo hautaweza kuwasilishwa mpaka bunge lijalo ambalo linatarajiwa kuwa mwezi wa nne.

Msigwa amesema hayo jijini hapa leo, Februari 7,2023 wakati akizungumza na waandishi wa habari ambapo amesema kutokana na ufinuyu wa muda wa shughuli za Bunge zinazoendelea hapa mjini Dodoma kwa wabunge kujadili taarifa ya Kamati za kudumu za Bunge imepelekea kusogeza mbele mswada wa Sheria ya huduma ya Habari uliofanyiwa marekebisho kutopelekwa bungeni kujadiliwa kama ilivyo stahili kuwa.

Kama mnavyojua ndugu zangu wanahabari Serikali baada ya kusikiliza maoni mbalimbali kutoka kwa wadau wa habari walitaka sheria ya huduma ya habari kufanyiwa marekebisho na kweli serikali ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassani aliona ni jambo jema ili kila mmoja aweze kufurahi na huduma hiyo

Kweli serikali imekusanya maoni na hata wanahabari walitoa maoni yao kwa kutokana na kupatikana kwa maoni Serikali ilikuwa imekusudia kupeleka marekebisho hayo bungeni ili wabunge waweze kujadili mswada huo,

 

Post a Comment

0 Comments