NSSF YAKUSANYA BILION 165.7 MAPATO YA UWEKEZAJI NA VITEGA UCHUMI VYA MFUKO

 ðŸ“ŒRHODA SIMBA

MKURUGENZI Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Masha  Mshomba amesema  katika nusu mwaka wa fedha iliyoishia  Disemba 2022, Mfuko umekusanya shilingi bilioni 165.7 kutokana na mapato ya uwekezaji na vitega uchumi vya mfuko. 

Mshomba amebainisha hayo leo Februari 8, 2023 Jijini Dodoma katika mkutano na waandishi wa habari wakati akielezea utekelezaji wa majukumu ya mfuko huo katika kipindi cha Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Amesema kiasi hicho cha mapato hakijajumuisha ongezeko la thamani ya vitega uchumi vya Mfuko huo na kuongeza kuwa katika kipindi husika thamani ya vitega uchumi vya Mfuko (investment portfolio) ilikua na kufikia shilingi trilioni 5.8 ikiwa ni ongezeko la asilimia 7 ikilinganishwa na thamani ya shilingi trilioni 5.4 iliyofikiwa katika mwaka wa fedha ulioishia mwezi Juni 2022.




 

Post a Comment

0 Comments