PATO LA TAIFA KUKUA KUPITIA UVUVI WA BAHARI KUU.

 ðŸ“ŒRHODA SIMBA

MKURUGENZI Mkuu wa Mamlaka ya kusimamia uvuvi wa bahari kuu Emanuel Sweke amesema  kwa kipindi cha mwaka 2022 hadi kufikia wiki mbili zilizopita uvuvi wa bahari kuu umeliingizia pato la taifa kiasi cha sh.bilioni 4.1.

Ameyasema hayo leo Februari 8 jijini Dodoma wakati akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa habari maelezo jijini Dodoma juu ya maendeleo ya mamlaka hiyo toka imeanzishwa kisheria mwaka 2010.

Dk.Sweke amesema kuwa licha ya kuwa Uvuvi ni gharama kubwa lakini umeweza kuliingizia pato taifa kwa njia za utoaji leseni kwa meli za ndani na nje ambazo zinataka kufanya biashara ya uvuvi katika bahari kuu.

Mamlaka ya kusimamia uvuvi wa bahari kuu umekuwa na majukumu mbalimbali ikiwa ni pamoja na utoaji wa leseni kwa meli ambazo zinatakiwa kufanya uvuvi na kuhakikisha zinapokuwa zimepewa leseni zinakuwa na bendera ya Tanzania.

Pamoja na kuwa na bendera ya Tanzania lazima kuwepo na usimamizi wa kulinda usalama wa wavuvi na meli zao huku tunahakikisha hakuna uvuvi haramu ambao umekuwa ukijitokeza katika bahari hiyo

Dk.Sweke.

Katika hatua nyingine amesema kuwa mamlaka katika kulinda usalama wa bahari kuu wameweka mifumo ya kulinda usalama ikiwa ni pamoja na kutumia mifumo ya kufuatilia meli ndani ya maji na kutumia doria za ndege kwa ajili ya kuangalia kinachofanyika.

Dk.Sweke amesema kuwa Mamlaka hiyo inatoa leseni kwa ajili ya uvuvi wa samaki aina ya jodari na kueleza kuwa inapotokea mwombaji anafanya tofauti hukamatwa.

Akizungumzia maendeleo ya mapato ndani ya bahari kuu amesema tayari mwekezaji kutoka nchini Uhispania anatarajia kujenga kiwanda cha kuchakata samaki ambacho kitajengwa katika bandari ya Tanga.

Amesema kuwa mpaka kiwanda hicho kikamilike kitagharimu kiasi cha dola milioni 10, kitazalisha ajira kwa watanzania 100 na kinatarajiwa kuchakata takribani tani 200 kwa siku.

Sambamba na hilo ameeleza kuwa bado mamlaka inakabiliwa na changamoto ya ajira ya moja kwa moja hivyo wapo katika mchakato wa kuanza kutao ajira kwa maafisa na waangalizi.

Aidha amesema toka Mamlaka kuanzishwa imefanikiwa kukamata meli moja iliyokuwa na samaki tani 100 ya samaki wasiolengwa.

 

Post a Comment

0 Comments