RAIS DK.SAMIA MGENI RASMI SIKU YA MARIDHIANO KITAIFA

 ðŸ“ŒRAHMA HAJIA

RAIS Dkt Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika siku kuu ya  Maridhiano Tanzania  inayotarajiwa  kufanyika Machi 3 katika ukumbi wa Jakaya Kikwete  ulipo  mkoani Dodoma

Hayo yameelezwa  leo  Februari 15 jijini  Dodoma   na Waziri Mkuu Mstaafu   Mizengo Pinda katika hafla ya uzinduzi wa Kamati ya Maridhiano itakayofanyika Machi 3 mwaka huu

Leo tumekutana hapa kwa ajili ya kuangalia hiyo siku ya maridhiano kitaifa tutaadhimisha kwa mambo yapi,mazungumzo yameshaanza  kwa kufanya mazungumzo na viongozi mbalimbali

Pinda.

Pinda ambaye  ndiye Mlezi wa Jumuiya ya Maridhiano Tanzania  amesema kazi kubwa  wanayofanya  ni kuzuia kuvunjika kwa  amani na utulivu kwa Taifa  na kutatua mifarakano kwa kukaa chini na kuyazungumza  ili yaishe.

Kwa upande wake Sheikh Alhad Mussa Salimu ameishukuru serikali ya awamu ya sita ya Dtk.Samia wanavyozidi kuunga mkono na kuahidi kuwa wataendelea kuchapa kazi ili watu wajua dhamira kuu ya jumuiya ya maradhiano.

Sisi  kama jumuiya ya maridhiano ni wajibu wetu kuhakikisha kwamba watanzania wanaishi kwa amani , upendo na  umoja na kuona kila mtanzania  naye ni mtu wa serekali ya jamhuri ya muungano wa Tanzania.

Naye Katibu wa Jumuiya ya Maridhiano Taifa  Israel Maasa  amesema kuwa jumuiya  hiyo imeendelea kujiimarisha na  kupinga suala la kupambana na ndoa ya jinsia moja kwani  ni mmomonyoko wa Maadili na inaenda kinyume na mila na desturi zetu za  kitanzania.   

Post a Comment

0 Comments