SERIKALI KUMALIZA CHANGAMOTO YA MAJI DAR, PWANI NA MOROGORO.

📌RHODA SIMBA

MKURUGENZI wa Bodi ya maji Bonde la Wami Ruvu  Mhandisi Elibarick Mmassy amesema  kuwa Serikali imejipanga kuhakikisha inamaliza changamoto ya tatizo la maji katika mikoa ya Dar es salaam,Pwani na Morogoro kwa kuchimba visima kumi vyenye maji ya kutosha.

Ameyasema hayo Leo Februari 7 2023 jijini Dodoma wakati akizungumza na waandishi wa habari   kuhusu utekelezaji wa miradi ya maji chini ya bodi hiyo.

Lengo la kuanzishwa kwa bodi ya maji ni pamoja na kuhakikisha rasilimali za maji zinalindwa, kutunzwa na kuendelezwa kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kizazi kijacho sambamba na kuhakikisha utunzaji wa mazingira

 

Post a Comment

0 Comments