SERIKALI YADHAMIRIA KUBORESHA UCHUMI WA VYOMBO VYA HABARI

 ðŸ“ŒJASMINE SHAMWEPU

NAIBU Waziri wa Habari,Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhandisi Mathew Kundo amesema serikali imedhamiria kuboresha uchumi wa vyombo vya habari hapa nchini ambapo kwasasa serikali imeunda kamati kuchunguza changamoto za kiuchumi katika vymbo vya habari ili serikali kushughulia changamoto hizo.

Mhandisi Mathew Kundo ameyasema hayo jijini Dodoma wakati akifungua mkutano wa mwaka wa watoa huduma wa sekta ya utangazaji Tanzania ambapo amesema serikali imedhamiria kuboresha uchumi wa vyombo vya habari hapa nchini.

Kwa upande wake mkurugenzi mkuu wa mamlaka ya mawasiliano Tanzania TCRA DKT.Jabir Bakari amesema jukumu la mamlaka hiyo ni kusimamia sekta ya habari huku akisisitiza kwamba sekta hiyo ina nafasi kubwa katika kutoa elimu kwa wananchi kuhusu uchumi wa kidigiti.

Naye mwakilishi wa IMAAN MEDIA Sheikh Mohamed Issa akichangia mada katika mkutano huo akaiomba mamlaka ya mawasiliano Tanzania TCRA kutoviwekea kikomo cha masafa ya kurusha matangazo vyombo vya kidini.

Katika mkutano huo unaofanyika kwa siku mbili jijini Dodoma ulioandaliwa na mamlaka ya mawasiliano Tanzania TCRA, umehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa vyombo vya habari akiwemo katibu mkuu wa Taasisi ya The Islami Foundition  inayomiliki vymbo vya habari ya imaan media Mussa Buluki


Post a Comment

0 Comments