TANESCO IMESEMA HALI YA UPATIKANAJI UMEME UMEIMARIKA NCHINI.

 ðŸ“ŒRHODA SIMBA

SHIRIKA la umeme Tanzania TANESCO limesema kuwa kwa sasa hali ya upatikanaji umeme imeimarika tofauti na ilivyokuwa mwaka 2022 kwani Serikali imeendelea na ujenzi wa miradi mbalimbali itakayoongeza kiwango cha uzalishaji nakuondoa adha ya wananchi kukosa huduma.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dodoma kuhusu utekelezaji wa shirika hilo kaimu mkurugenzi huduma kwa wateja shirika la umeme TANESCO Martin Mwambene amebainisha baadhi ya miradi hiyo kuwa ni mradi wa bwawa la Nyerere, miradi ya gas na miradi ya jua itakayofanyika Dodoma, Singida na Shinyanga itawezesha kuongeza kiwango cha uzalishaji wa umeme kufikia megawati 5000 mwaka 2025.

Akizungumza kuhusu upatikanaji wa umeme amesema uwezo wa kuzalisha umeme ni megawati 1820 na kiwango kinachopatikana ni megawati 1300 huku akieleza kuwa uzalishaji huu unasababishwa na mapungufu yaliyopo kwenye uzalishaji na hitilafu kwenye mitambo.

Naye Msemaji Mkuu wa Serikali na Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo Gerson Msigwa amesema nishati ya umeme ni muhimu na ni hitaji la msingi na lazima kwa kila mtu ndio maana serikali inahakikisha huduma hiyo inawafikia wananchi wote popote walipo.



Post a Comment

0 Comments