TANESCO YATOA MKAKATI KUKATIKA KWA UMEME

 ðŸ“ŒGETRUDE VANGAYENA 

KAIMU Mkurugenzi wa nishati huduma kwa wateja Martin Mwambene ameelezea sababu zinazopelekea umeme kukatika mara kwa mara hali inayopelekea kukwamisha baadhi ya shughuli za wananchi kushindwa kuendelea. 

Akizungumza na waandishi wa habari  leo amesema  sababu zinazopelekea  kukatika kwa umeme  ni pamoja na  mvua za vuli kuwa chache hali inayosababisha kushindwa kuzalisha megawati nyingi za umeme .

Amesema kutokana na changamoto hiyo wameweka mipango mikakati ambayo itaweza kuzalisha megawati nyingi tofauti na zamaniAmesema kuwa kwasasa wanazalisha megawati 1300 wakiwa na lengo la kufikia  megawati 5000 mwaka 2025

Kwa sasa tunajitahidi kufikia megawati 5000 hadi kufikia mwaka 2025 tatizo la umeme litakua limeisha.

Lakini kwa sasa umeme umekua sawa kwa maana kwamba umeme hausumbui, kwa sasa tumepungukiwa megawati  70 tu na hii yote ni kutokana na kugundua sababu inayochangia kukatika umeme  na kuweza kutenga shilingi bilioni 4 kwaajili ya marekebisho zaidi.

 Pia amesema wana ujenzi wa kupooza umeme wa vituo vikubwa na uzalishaji wa ubora wa miundombinu kwaajili ya kumaliza changamoto za umeme. 

 

 

Post a Comment

0 Comments