WAKUU WA MIKOA, WILAYA WATAKIWA KUSIMAMIA SERA YA AFYA

📌 RHODA SIMBA

NAIBU WAZIRI wa Afya Dkt. Godwin Mollel ametoa wito kwa viongozi ngazi ya Mkoa na Wilaya kushirikiana kwa karibu kusimamia takwa la kisera linaloelekeza huduma bure kwa watoto chini ya miaka mitano na wajawazito. 

Dkt. Mollel ameyasema hayo leo Februari 7, 2023 wakati akijibu swali la Mbunge wa Temeke Mhe. Dorothy Kilave katika Mkutano wa kumi kikao cha sita, Bungeni Jijini Dodoma. 

Suala hili ni la kisera kwamba, mama mjamzito na watoto wa umri chini ya miaka mitano hawatakiwi kulipishwa, hivyo niombe Wakuu wa Wilaya na Wakau wa Mikoa tuweze kushirikiana kwa pamoja kusimamia hili takwa la kisera.

Dkt. Mollel.

 

Post a Comment

0 Comments