WATANZANIA LAKI NANE KUSHIRIKI SOKO LA PAMOJA LA FEDHA

📌RHODA SIMBA

MKURUGENZI Mtendaji wa taasisi ya Watumishi Housing Investment (WHI), Dkt.Fred Msemwa amebainisha ,watanzania 80000 ndio wanaoshiriki katika uwekezaji wa pamoja wa soko la fedha.

Hivyo watanzania wameshauriwa kujitokeza kujiunga na mfuko wa Faida Fund ambao utawawezesha kufikia malengo, kujiletea maendeleo na kujikwamua kiuchumi.

Dkt.Msemwa amebainisha hayo leo Februari 9, 2023 jijini Dodoma wakati akieleza utekelezaji wa Majukumu ya Mfuko huo katika mkutano wake na waandishi wa habari.

Amesema kuwa kupitia Mfuko wa Faida Fund ambao unatumia mfumo wa malipo ya Serikali wamevuka lengo kwa kukusanya michango ya Sh. bilion 12 .9 katika mauzo ya awali huku matarajio yalikuwa ni kukusanya Sh.bilioni 7 ikiwa ni ndani ya miezi miwili tangu kuanzishwa kwake.

Hapa nchini watanzania 80000 ndio wanaoshiriki katika uwekezaji wa pamoja wa soko la fedha, hivyo nawashauri watanzania kujitokeza kujiunga na mfuko huo ambao utawawezesha kufikia malengo, kujiletea maendeleo na kujikwamua kiuchumi

Dkt.Msemwa

Mkurugenzi huyo amesema makusanyo hayo ya Mfuko ni katika kipindi cha Novemba mwaka jana mpaka kufikia Februari 9 walikuwa na Sh.bilioni 14, na kwamba fedha hizo wameziwekeza katika masoko ya fedha ikiwemo mabenki na Serikali ambapo watanzania zaidi ya 4000 wamejiunga.

Kuhusu uendeshaji wa Mfuko huo, amesema Faida Fund unafanya kazi kwa njia ya kuuza vipande, ambapo bei ya kipande ilikuwa sh 100, mpaka sasa thamani ya kipande imefikia sh 101.1, hivyo thamani ya vipande imeendelea kukua.

Akizungumzia uuzaji wa vipande mkurugenzi huyo amesema, Watumishi Housing ndio wanaonunua vipande kutoka kwa wawekezaji ambao ni wanachama wa Mfuko huo watakaokuwa na uhitaji wa kuuza vipande vyao ili wapate Fedha.

Dkt. Msemwa ametaja faida ya kuwekeza kwenye Mfuko, kuwa ni pamoja na kuwa na uwezo wa kuwekeza katika masoko ya Fedha bila kulazimika kufuata mlolongo mrefu ikiwemo kwenda kwa madalali, uwekezaji hufanyika kwa njia ya simu hivyo kuokoa muda na kuwa na usalama wa fedha na kupata unafuu na kuwekeza bila tozo huku uwekezaji wako ukitambulika kwa kasi kubwa.

Pia amesema uwekezaji unaweza ukautumia kama dhamana pale utakapohitaji mkopo wa Benki ili kujiongeza zaidi kiuchumi na Mfuko wa Faida Fund ni endelevu na unalenga sekta zote.

Kuhusu ujenzi wa nyumba amesema Nyumba 983 tayari zimejengwa kupitia taasisi hiyo ya Watumishi Housing nchi nzima na kwamba katika ujenzi wa kila nyumba 100 Watumishi Housing huzalisha ajira kwa watu 120 hapa nchini

 


 

Post a Comment

0 Comments