BRELA: WATAALAMU WA VYOMBO VYA UCHUNGUZI WATAKIWA KUFANIKISHA MKATABA WA KUDHIBITI NA KUPAMBANA NA UTAKATISHAJI WA FEDHA HARAMU.

 JASMINE SHAMWEPU

MKURUGENZI wa Idara ya Kampuni na Majina ya Biashara kutoka BRELA, Meinrad Rweyemamu amesema wataalamu wa vyombo vya uchunguzi wametakiwa kuhakikisha wanafanikisha mkataba wa taifa wa kudhibiti na kupambana na utakatishaji wa fedha haramu, ufadhili wa ugaidi , ufadhili wa silaha za maangamizi na kuhakikisha nchi inatoka kwenye Grey List ya FATF.

Rweyemamu ameyasema hayo leo jijini Dodoma wakati wa kikao cha majalidiliano kuhusu utekelezaji wa kanuni za wamiliki manufaa baina ya wakala na vyombo vya uchunguzi  kwa niaba ya Afisa Mtendaji Mkuu wa BRELA Godfrey Nyaisa.

Aidha Rweyemamu amewataka wataalamu hao kuhakikisha wanafanikisha mkataba wa taifa wa kudhibiti na kupambana na utakatishaji wa fedha haramu.

Amesema wakala  ilitoa access ya mifumo yetu ya ndani ikiwemo mfumo wa usajili kwa njia ya mtandao na mfumo wa wamiliki manufaa kwa vyombo vya uchunguzi,”amesema Rweyemamu

Aidha Rweyemamu, amesema BRELA  imekuwa ikishirikiana kwenye shughuli mbalimbali za kiutendaji ikiwa ni pamoja na kufanya maboresho mbalimbali ya kisheria na kimfumo ili kuhakikisha wanatoa  huduma bora.

Amesema Benki ya Dunia na taasisi zingine zimejitolea kuleta mabadiliko ya hali hiyo kwa kuanzisha dhana ya wamiliki manufaa ambayo imeungwa mkono na Jumuiya ya Kimataifa.

Amesema kwa kuwezesha juhudi hizo Taasisi ya Kimataifa ya Financial Action Task Force (FATF) mwaka 2014 ilitoa muongozo kwa taasisi ya Kimataifa ya Globar forum on Transparency and Exchange of Information for Tax Purposes.

Kwa upande wake, Kaimu Kamishna wa Uhamiaji, Charles Kasambula amesema mafunzo hayo ni muhimu kutokana na dunia ilivyo kwenye suala zima la utakatishaji fedha.

Kama nchi ni vyema tukapata mafunzo haya na sisi kama wahamiaji wawekezaji lazima wapite kwetu ili kuweza kupata vibali vya kuishi na kuwa na makazi nchini, hivyo itasaidia watu wanapoanzisha kampuni zao hasa wa nje kuweza kuchunguza vyanzo vya pesa zao ili tuwe na watu safi sio watu wanaotaka kutakatisha pesa zao.

 

Post a Comment

0 Comments