DK.MPANGO KUZINDUA MCHAKATO DIRA YA TAIFA 2050

 ðŸ“ŒJASMINE SHAMWEPU

MAKAMU wa Rais Dk. Philip Mpango, anatarajiwa kuzindua mchakato wa maandalizi ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 ambayo itatoa maono na kuweka malengo ambayo taifa linataka kuyafikia ndani ya kipindi cha miaka 25 ijayo.

Naibu katibu mkuu wizara ya Fedha na Mipango Jenifer Omolo, alibainisha hayo alipokuwa akitoa taarifa kuhusu uzinduzi wa mchakato huo kwa waandishi wa habari ambao unatarajiwa kufanyika April 3, mwaka huu jijini hapo.

Dira hii itatoa maono na kuweka malengo ambayo taifa letu linataka kuyafikia ndani ya kipindi cha miaka 25 ijayo baada ya kuisha kwa kipindi cha utekelezaji wa Dira tuliyo nayo sasa ya Taifa ya Maendeleo 2025.

Maandalizi ya Dira mpya ya 2050 yanakidhi matakwa ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambayo ndio mwongozo mkuu wa nchi yetu

Omolo

Aidha, amesema mnamo mwaka 2009/10, serikali ilifanya tathmini ya utekelezaji wa Dira 2025 kupitia mikakati na programu za maendeleo. Amesema tathmini hiyo ilibainisha uhitaji wa Taifa kuanza kupanga vibaumbele vya nchi.

Suala hili lilipelekea kuandaliwa kwa Mpango Elekezi wa Maendeleo wa Muda Mrefu (LTPP) 2011/12 - 2025/26)

Omolo

Vile vile, amesema Mpango huo wa miaka 15 ulipangwa kutekelezwa kwa mipango ya muda wa kati ya miaka mitano na mipango ya muda mfupi ya mwaka mmoja.

Ndugu wanahabari, katika utekelezaji wa Dira ya Maendeleo ya Taifa ya mwaka 2025, Taifa limeweza kupiga hatua kubwa ya maendeleo katika nyanja mbalimbali hususani za kijamii, kiuchumi na kisiasa.

Hata hivyo, utekelezaji wa Dira  2025 unafikia tamati mwaka 2025.  Kwa msingi huo, ni jukumu letu sote kwa nafasi zetu kuanza kufikiria juu ya mafanikio ya utekelezaji wa dira 2025 na  mustakabali wa nchi yetu katika miaka ya mbele ijayo

Kadhalika, amesema ili kufanikisha maandalizi ya  Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 kunategemea kwa kiasi kikubwa ushiriki wa wadau wote.

Hivyo, nitoe rai kwa wadau wote katika maeneo yao kushiriki kikamilifu katika kutoa mchango wao utakaowezesha kuandaliwa kwa Dira yenye maono ya watanzania kwa miaka 25 ijayo

Omolo

 

Post a Comment

0 Comments