DKT. GWAJIMA:SERIKALI KUWAWEZESHA WANAWAKE KIUCHUMI

 📌GETRUDE VANGAYENA & RAHMA HAJIA

SERIKALI kwa kushirikiana na wadau imedhamiria kuwawezesha wanawake kiuchumi ili kuwakwamua kutokana na changamoto zinazowakabili ikiwemo mila na desturi.

Hayo yamesemwa  jijini Dodoma na Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi maalum Dkt Dorothy Gwajima  wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana  na maadhimisho ya kilele cha siku ya wanawake duniani inayofanyika machi 8 kila mwaka.

Amesema  ni muhimu  kuwepo na usawa kwa wanawake  kutokana  na hatua ambazo wanazichukua ili kuwasaidia wanawake  kwa kuwawezesha ili kujikwamua kiuchumi kutokana na changamoto wanazokabiliana nazo katika jamii.

Amesema  kuwa changamoto hizo  ni pamoja na vikwazo vya mila na desturi ambazo zinawakumba zaidi wanawake wenye umri mkubwa ,walemavu  na wanawake  wanaoishi vijijini.

Serikali imeamua kushirikiana na wadau ili kuwawezesha wanawake  kiuchumi, teknolojia  na kidigitali ili kuwanufaisha wanawake  waweze kuwa na matumizi sahihi ya kimtandao

Amesema  kuwa takwimu za dunia kuhusu kamisheni ya wanawake inaonesha kuwa wanawake  na wasichana hawanufaiki na matumizi ya teknolojia ikiwa mwaka 2022 asilimia 67 ya wanawake  wanaotumia mtandao na asilimia  69 ni wanaume ambapo ni sawa na asilimia 12 ukilinganisha na  wanawake ni wachache. 

Pia amesema  kuna umuhimu  wa kuenzi mawazo ya kijasiri yenye kuleta mabadiliko ya kuchochea teknolojia ikiwa ulimwengu  wa leo wa karne ya 21 upo kwenye zama za kidigitali ambayo inachochea chachu yenye kuleta maendeleo kwa wanawake. 

Hata hivyo Gwajima ametoa wito kwa wanawake kujitokeza kwa wingi katika siku ya maadhimisho ya siku ya wanawake chini ya wakuu wa mikoa wakiwa na vazi la batiki kila mtu kwa uwezo wake.

 

 

Post a Comment

0 Comments