JAMII YASHAURIWA KUACHA KUKOPA MIKOPO UMIZAA

 📌JASMINE SHAMWEPU

JAMII  Imeshauriwa kuacha kukopa mikopo umiza Maarufu kama KAUSHADAMU, Vishoka na mikopo yote inayofanana na mikopo hiyo kwani mikopo hiyo ni uhalifu katika nchi na badala yake wametakiwa kufuatilie taarifa zinaazotolewa na benki za watoa huduma wadogo  wenye leseni.

Hayo yameelezwa jijini Dodoma na Mary Ngasa Afisa Mkuu katika Idara Ndogo za Fedha kutoka Benki Kuu ya Tanzania kwenye kikao kilichowakutanisha wamiliki na wakurugenzi wanaotoa huduma ndogo za kifedha nchini.

Afisa huyo amesema kupitia kanuni wale wote waliosajiliwa wanatambulika na kwa wale wanaotoa huduma ndogo za fedha bila kutambulika yani Kutoa huduma ya Fedha bila kuwa na leseni ya Benki Kuu wanafanya uhalifu na kuvunja sheria za nchi pale watakapo kamatwa hatua Kali zitachukuliiwa ikiwemo kukamatwa na kufikishwa mahakamani.

Kwa sababu kitu wanachokifanya ni kinyume cha sheria kwani wanatoa huduma bila Usimamizi Wala ukaguzi  wakati huduma za fedha ni huduma nyeti na taarifa zote nyeti kama huduma ya fedha zinasimamiwa na benki kuu kutoa huduma ya Fedha bila kufuta Muongozo wa benki Kuu ni kinyumbe cha sheria

Mkitaka mkopo angalia mtoa huduma anayetoa huduma ana leseni msichukue mikopo mitaani ni kweli wanawaumiza Wananchi kwani hawasimamiwi, hawajali anaweza kukuumiza na kutokomea pasipo julikana,"

Aidha Afisa huyo alitoa ufafanuzi kuwa baadhi ya kanuni, mitaji ya sheria pia kanuni ya kusimamia sheria za walaji ambazo watoa huduma katika kikao hicho walijadili TAMIU walipeleka mawazo na changamoto zao ambazo wamejadiliana huku Afisa huyo kuyapeleka kwa njia ya maandishi Benki Kuu.

Naye Mwenyekiti wa Tanzania Microfinance Union (TAMIU) Juma Mnaka Mkurugenzi wa kampuni ya Mnaka Microfinance  Sumbawanga  wamekubaliana watoa huduma wadogo wa fedha kufuta sheria za Utoaji wa mikopo sheria ya mwaka 2019 na Kanuni zake wafanye kazi kwa kushirikiana na serikali kwa kuchangia Kodi kwa mujibu na Sheria ili kuinua Pato la Taifa na serikalli kupata fedha ili ilete Miradi katika nchi yetu.

Pia katiki kikao hicho wamekubaliana wakurugenzi wote kuchangia ushuru kwenye Halmashauri ili kuziinua na kuweza kuleta Maendeleo .

Kwa upande wake Katibu wa  TAMIU Wambura Sasi Ilumbe amesema wao Kama TAMIU wamesajiliwa 2020 mwezi wa Sita  na wanachama wake wapo 255 Wilaya zote za Tanzania bara ambapo tayari wameshatoa ajira 2925.

Sisi ni muhimu katika nchi kwani tumeweza kupunguza tatizo la ajira kwa watanzania wenzao pia kwa umoja wao wamekuwa wakipata huduma ya moja kwa moja kwa wale wanaowa wasimimia yani Benki Kuu hivyo wanapata urahisi wa kuwapata kwa pamoja niwaombe makampuni mingine yaliosajiliwa na kibali cha benki kuu kujiunga na umoja huo kwa ajili ya kuwa na nguvu na kupata taarifa ya pamoja na kwa haraka zaidi.

 

Post a Comment

0 Comments