JWTZ YATANGAZA NAFASI ZA KUJIUNGA NA JESHI.


📌RHODA SIMBA

JESHI la Wananchi Tanzania  limetangaza nafasi za kujiunga na jeshi kwa vijana wa kitanzania wenye elimu ya kuanzia kidato cha nne hadi shahada ya uzamili ambao wamemaliza mkataba  wa miaka miwili wa mafunzo ya kujitolea  katika jeshi la kujenga taifa na kurudishwa majumbani.

Akitoa taarifa hiyo kwa waandishi wa Habari leo Machi 9 2023 Jijini Dodoma Kaimu Mkurugenzi wa Habari   na uhusiano wa JWTZ, Luteni Kanali GAUDENTIUS ILONDA, amesema nafasi hizo zinawahusu  vijana wenye umri kuanzia miaka 18 hadi 26 kwa  wenye elimu ya kidato cha 4 na cha sita na umri usiozidi miaka 27 kwa wenye elimu ya juu.

Aidha, Luteni Kanali ILONDA, ameeleza vigezo vitakavyozingatiwa wakati wa maombi hayo kuwa mwombaji awe raia wa Tanzania wa kuzaliwa mwenye kitambulisho cha Taifa, awe na afya nzuri na akili timamu, awe na cheti halisi cha kuzaliwa, vyeti vya shule na vyeti vya taaluma.

Vigezo vingine ni pamoja na na awe hajatumikia Jeshi la Polisi, Magereza, Chuo cha Mafunzo au Kikosi maalumu cha kuzuia magendo na asiwe ameoa au kuolewa.

Sambamba na hayo amewataka wananchi kutorubuniwa na Matapeli bali Jeshi la wananchi halijuani na mtu yoyote yule.

Kwa upande wa utaratibu wa jinsi ya kutuma maombi Luteni Kanali Ilonda, amebainisha kuwa maombi yote yaandikwe kwa mkono na yawasilishwe makao makuu ya Jeshi hilo Dodoma kuanzia leo tarehe 9, Machi hadi tarehe 20, Machi 2023 yakiwa na viambatanisho kama vile nakala ya kitambulisho cha taifa au namba ya nida, nakala ya cheti cha kuzaliwa, vyeti vya shule na chuo, nakala cheti cha JKT na namba ya simu ya mkononi ya muombaji

  

Post a Comment

0 Comments