SHIRIKA LA TYVA LAWAKINGIA KIFUA VIJANA.

 📌RHODA SIMBA 

Katika kuelekea bajeti ya mwaka wa fedha 2023/24 Shirika lisilo la Kiserikali la Vijana kupitia mradi wa vijana makini (TYVA) limeiomba Serikali katika mikopo inayotolewa na Halmashauri kwaajili ya Vijana iongezwe asilimia nne ili kuwasaidia kuweza kujikwamuwa kiuchumi .

Akizungumza Jijini Dodoma Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la vijana kupitia mradi wa vijana makini (TYVA) Yusuph Bwango amesema Serikali inapaswa kusimamia maeneo ya uwezeshaji wa kifedha na mikopo yenye masharti nafuu lengo ni kuwainua vijana kiuchumi kupitia mikopo ya Halmashauri.

Tunatambua serikali imefanya kazi kubwa sana kuhakikisha kwamba mikopo ya Halmashauri ya asilimia 4 inaenda kwa vijana kwa wingi lakini vijana walitamani kuona ile mikopo ikiongezeka na masharti yake yaweze kuwa nafuu zaidi kuweza kuwafanya vijana waweze kujikwamua kiuchumi na kuendesha shughuli zao za kijasiliamali na kiuchumi kwa upana

Pia amesema kuwa vijana wameguswa na tozo zilizowekwa na Wizara ya Fedha kwa kupitia sheria ya fedha na kwamba vijana wameomba kupitia bajeti ya mwaka 2023/24 serikali iweke tozo himilivu kwa vijana na kuangalia sekta zingine ambapo Serikali itaweza kukusanya fedha kwaajili ya kufidia bajeti ya serikali.

Katika tafiti tumeweza kuona Serikali kwa mwaka inakadiriwa kupoteza zaidi ya Dola bilin 7.6 ukichukua asilimia 20 ya fedha ambayo Serikali inapoteza kupitia michakato mbalimbali ya kikodi inaweza ikalipa zaidi ya walimu laki moja na themanini Nchi nzima wa shule za msingi na awali,

Serikali inaweza ikajenga Madarasa zaidi ya 200,000 Nchi nzima kama zikitumika zile fedha ambazo zinapotea kwahiyo vijana wanaona Serikali kuna haja ya kuongeza nguvu kwenye maeneo ambayo inapoteza hela kwa wingi na kupunguza maeneo ambayo vijana wanaumia sababu maeneo hayo yakikusanya fedha kwa wingi vipaumbele vya vijana vitatatuliwa pamoja na changamoto zao

Naye Fred Mtei mtetezi wa vijana kutoka Taasisi ya Maendeleo ya Vijana amesema kuwa kutokana na uchambuzi walioufanya uliwalenga vijana sababu vijana ni asilimia 34.5 inayokadiriwa kuwa asilimia 35 na wanachangia nguvu kazi ya Taifa kwa asilimia 64.5 na kuwa ni kundi kubwa katika Taifa kwa mujibu wa takwimu za NBs.

Amesema kuwa vijana ndio kundi kubwa linalochangia katika nguvu kazi ya Taifa na ukizungumzia Taifa huwezi acha kuzungumzia kundi la vijana ndio sababu wamejikita katika kundi hilo.

Kwa upande wake Dkt.Thea Mtala Mbunge muwakilishi wa vyuo vikuu amesema kuwa kutokana na kuwepo kwa tatizo la utafiti ni muhimu Serikali ikabuni na kuweza kupata vijana katika kila Wizara au sekta ambao watakuwa wanafanya tafiti kwa urahisi na wepesi na kupeleka majibu katika Serikali ili iweze kuona namna ya kufanya ufumbuzi katika tafiti hizo.

Amesema kuwa kumekuwa na tamaduni ya kuziachia Wizara zifanye tafiti zenyewe kitendo kinachopelekea tafiti nyingi kutopata ufumbuzi.

Ni vizuri pia Serikali ikabuni kupata vijana katika kila Wizara au katika kila sekta ambao watakuwa wanaweza kufanya tafiti zetu kwa urahisi na wepesi na kupeleka majibu katika Serikali ili Serikali iweze kuona namna gani sasa itafanya ufumbuzi katika eneo hilo la utafiti hasa kama utafiti huo tayari umetoa mapendekezo yakapelekwa katika kila Wizara itakuwa ni rahisi

 

 

 

Post a Comment

0 Comments