TASAC KUKAMILISHA MRADI WA KIMATAIFA ZIWA VICTORIA

 📌RHODA SIMBA

KATIKA kuboresha sekta ya usafiri wa maji Shirika la Uwakala wa meli Tanzania (TASAC) limeweza kuunda nyenzo za udhibiti wa huduma za usafiri kwa njia ya maji pamoja na kukamilisha mradi wa kimataifa wa mawasiliano na uchukuzi katika Ziwa Victoria ambao utagharimu bilioni 59.23.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Machi 7 jijini Dodoma Mkurugenzi Mkuu wa TASAC Kaimu Mkeyenge amesema tangu kuanzishwa kwake inajivunia mambo mengi sana hususani juhudi za Serikali katika kuboresha sekta ya maji.

Aidha amesema Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania limeendelea kuimarisha miundo mbinu ya mfumo wa Tehama ikiwemo ambazo zinasaidia kukusanya mapato na huduma za biashara ya meli.

 

Post a Comment

0 Comments