TASAC YAENDASHA MPANGO WA KUZUIA UMWAGIKAJI MAFUTA BAHARINI

 📌RAHMA HAJIA & GETRUDE VANGAYENA .

SHIRIKA la Uwakala wa Meli  Tanzania (TASAC)  limearatibu mpango wa Taifa wa kuzuia na kupambana na Umwagikaji wa  mafuta baharini ili kulinda mazingira pamoja na viumbe hai vinavyopatikana baharini

Akizungumza na wanahabari leo jijini Dodoma katika kueleza utekelezaji wa majukumu ya Shirika la Uwakala wa Meli nchini  Mkurugenzi mkuu wa shirika hilo Bw Kaimu Abdi Mkeyenge amesema kuwa wameweza kukabiliana na changamoto ya umwagikaji mafuta  ambapo inahatarisha maisha ya viumbe hai waishio baharini .

Amesema pia shirika hilo linajihusisha na utekelezaji wa mikataba, itifaki na miongozo inayotolewa na Shirika la Bahari  duniani (IMO) kwa niaba ya nchi inaporidhia ambapo hadi sasa imeridhia usainishwaji wa mikataba 24 inayojumuisha mikataba mikuu 6 ya lazima.

Shirika limeimarisha udhibiti wa usalama na ulinzi kwenye maeneo ya shughuli za bandari kwa kusimamia urasimishaji wa maeneo 20 ya kibandari katika mwambao wa bahari na maziwa kama vile Somanga-Lindi, Kunduchi-Dar es salaam na Kilongwe- Mafia,’’amesema.

Pia shirika  limeweza kukagua meli za nje zinazofika katika  bandari zetu  ambapo kwa kipindi cha kuanzia Julai 2022 hadi Disemba 2022 imekagua meli za kigeni 36 na kuanzia Januari 2023 imekagua meli za kigeni 37 ambapo shirika linategemea kukagua meli 61 hadi kufikia Juni 2023.

Licha ya hivyo pia shirika limesaidia katika ongezeko la idadi ya vyeti vya mabaharia waliokidhi masharti kutoka 6068 katika mwaka 2018/19 hadi kufikia 19575 katika mwaka 2021/22 sawa na  ongezeko la asilimia 31

Hata hivyo kutokana na mafanikio yaliyopatikana katika kipindi hicho lakini kuna fursa mbalimbali katika sekta ya usafiri majini ambazo zinaweza kukuza uchumi na kuongeza ajira kwa wananchi kama vile kuanzisha utaratibu wa kusajili meli kwa masharti nafuu.  

 

Post a Comment

0 Comments