UBUNIFU WA MABADILIKO YA TEKNOLOJIA CHACHU KATIKA KULETA USAWA WA KIJINSIA

📌MWANDISHI WETU

MKUU wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule ameshiriki katika hafla ya ugawaji majiko Banifu 114 yanayotumia nishati safi na Salama ya kupikia katika hafla iliyofanyika Wilaya ya Bahi Kijiji cha Zanka ambapo wananchi wa kijiji hicho na kijjii cha Kigwe wamenufaika. Majiko hayo yametolewa na jumuiya ya wanawake ya wakala wa Nishati Vijijini ambao ndio waandaaji wa tukio hilo ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani.

Akizungumza na wananchi wa vijiji hivyo, Senyamule amesema kuwa Matumizi ya kuni na Mkaa yamekuwa chanzo kikuu kinachotumika kwa kupikia hususani Maeneo ya Vijijini na kupelekea kutumika kwa kiwango kikubwa na hivyo kuleta athari katika mazingira.

Serikali itaendelea kuweka vivutio kwa wazalishaji na wasambazaji wa Teknolojia na bidhaa za nishati safi na salama ya kupikia na kuongeza wigo wa upatikanaji wa bidhaa pamoja na kutoa unafuu wa gharama ili kuwezesha watumiaji kutumia bidhaa hiyo

Mhe. Senyamule.

Zaidi ya tani milioni mbili za Mkaa zimekuwa zikitumika kwa mwaka kama nishati ya kupikia hivyo imeleta athari za mazingira na afya katika jamii, zaidi ya asilimia 85 ya kaya hapa nchini hutumia kuni na Mkaa kama chanzo kikuu cha nishati ya kupikia.

Naye Mkurugenzi Uendelezaji Masoko na Teknolojia Wakala wa Nishati Vijijini (REA) Bi. Advera Mwijage amesema jiko linatumia nishati mbili ambayo ni jiko la kuni na mkaa ambalo linaweza kutumika sehemu yoyote na inamsaidia mwananchi au mama wa kitanzania kupunguza gharama ya matumizi ya fedha na kupunguza ukataji wa miti ovyo.

Vilevile Mwenyekiti wa kijiji cha Kigwe Jeremia E.Sobayi amesema kila mwananchi  anatakiwa kuwa balozi mzuri  katika matumizi  sahihi ya majiko hayo na kila mmoja wao awe mlinzi wa mwenzake ili isije kutokea mtu akafanyia matumizi mengine nje ya malengo yaliyowekwa ya kutunza mazingira kwa kutokukata miti hovyo.



 

Post a Comment

0 Comments