MAJALIWA AIPONGEZA WIZARA YA MAJI UTEKELEZAJI MIRADI

 

📌RHODA SIMBA

WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa ameisifu Wizara ya Maji kwa kuendelea kutekeleza miradi mbalimbali ya maji, hasa kwa kufikisha miradi hiyo kwenye ngazi ya vitongoji nchini.

Ameyasema hayo jijini Dodoma wakati akifungua Semina kwa wabunge kuhusu Sekta ya Maji ambapo amesema Wizara hiyo imetekeleza maagizo ya ilani ya CCM pamoja na maelekezo ya Rais Samia Suluhu Hassan aliyotoa wakati anafungua bunge mwaka 2021.

Waziri Mkuu amesema Wizara hiyo, imefanya maboresho mbalimbali kwenye halmashauri kwa kubadili mfumo wa utoaji huduma ya maji kwa kuunda Mamlaka ya Maji Vijijini (RUWASA) ambayo ina jukumu la kusimamia na kusambaza maji kwa uhakika katika ngazi za wilaya hadi vijijini.

Amesema Wizara kwa kuweka mpango kazi wake imeweza kutekeleza na kukamilisha miradi mipya na imekwamua miradi iliyokwama na kuhakikisha inafanya kazi na kutoa huduma ya maji kwa wananchi.

Kwa kutekeleza miradi hiyo, imesaidia binadamu na viumbe mbalimbali vinavyohitaji maji kupata huduma hiyo katika maeneo yao.

Waziri Mkuu amesema Wizara hiyo, imefanya maboresho mbalimbali kwenye halmashauri kwa kubadili mfumo wa utoaji huduma ya maji kwa kuunda Mamlaka ya Maji Vijijini (RUWASA) ambayo ina jukumu la kusimamia na kusambaza maji kwa uhakika katika ngazi za wilaya hadi vijijini.

Kampeni ya kulinda vyanzo vya maji inatakiwa kuwa shirikishi zikiwemo ofisi ya Rais, Makamu wa Rais na wizara, taasisi na idara mbalimbali ili wizara ifanikishe azma yake ya kufikisha maji hadi kwenye vitongoji.

Waziri wa Maji, Jumaa Aweso amesema, wizara hiyo imejipanga vizuri kuondoa kadhia za maji nchini na imefanikiwa kutekeleza hilo kutokana na Rais Samia Suluhu Hassan kutoa fedha za kutosha katika kutekeleza miradi mbalimbali ya maji nchini.

Aweso amesema wizara hiyo itahakikisha inatekeleza maagizo ya Ilani ya CCM ya kusambaza maji hadi ifikapo mwaka 2025 kwa asilimia 85 vijijini na mjini kufikia asilimia 95, akaahidi wizara hiyo kutokuwa kikwazo kufikia malengo hayo.

 

Post a Comment

0 Comments