DC SHEKIMWERI AONGOZA ZOEZI LA UKAGUZI MATUMIZI YA MASHINE ZA EFDS KWA WAFANYABIASHARA

 ðŸ“ŒRHODA SIMBA

MKUU wa Wilaya ya Dodoma Mjini Jabiri Shekimweri ameongoza zoezi la kupita katika maeneo mbalimbali ya kuhamasisha matumizi ya mashine za kielektroniki (EFDs)  kwa wafanyabiashara akiwa na baadhi ya viongozi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa kikodi Dodoma,  kwa lengo la kutoa elimu kwa wafanyabiashara  juu ya matumizi ya mashine hizo.

Akizungumza mara baada ya kukagua baadhi ya maduka katika eneo la Meriwa lililopo jijini Dodoma Shekimweri amesema yeye kama Mwenyekiti wa kamati ya kodi Wilaya, moja kati ya  maazimio ya vikao vyao ni  kukumbushana kuwa nao wanao  wajibu wa kupita kuhamasisha, kukagua,na  kukumbusha matumizi ya mashine hizo za EFDs

Kampeni hii ni ya mwezi mzima tunataka kuona muitikio wa wananchi upoje kwasababu matumizi yake hupelekea kodi na mapato mbalimbali ya Serikali kuweza kupatikana, lakini pia  tumepita kuona changamoto zao lakini tumefarijika kuona matumizi ni mazuri

Shekimweri 

Naye Meneja  Msaidizi wa TRA Mkoa wa  Dodoma  Ramadhan Sengo amesema Mamlaka imeanzisha  kampeni ya TUWAJIBIKE  lengo  ni kuhamasisha wauzaji kutoa risiti  halali na wateja kudai risiti inayoonesha kiwango halali walicholipa.

Kutokutumia mashine za EFDs  ni kosa kisheria tutakapomkuta mtu hatumii adhabu lazima akutane nayo 

Kwa upande wake Rajabu Kibwana  mfanyabiashara  katika eneo hilo la Meriwa amesema kama wananchi pia  wanao wajibu wa kutumia mashine hizo bila kukumbushwa na Mamlaka husika  kwakuwa  faida  ya  utoaji kodi  ndio chanzo cha ujenzi wa  baadhi ya miradi ya maendeleo  inayofanywa hapa nchini.

Hakuna mtu atakaye tujengea nchi zaidi ya sisi wananchi wenyewe ujenzi wa barabara  shule na mambo mengine yote yanayofanywa na mama yetu Rais Samia Suluhu Hassan  yamefanywa  kupitia kodi zetu hivyo sisi kama wananchi tunao wajibu  wa kutoa kodi kwa kupitia mashine hizi za (EFDs) 

Kibwana



 

Post a Comment

0 Comments