JAJI MKUU AMEITAKA MAHAKAMA SAFARI YA KUHAMIA DODOMA IFANYIKE KIDIGITALI

 ðŸ“ŒJASMINE SHAMWEPU

JAJI Mkuu Profesa. Ibrahim Hamis Juma ameitaka mahakama kuhakikisha safari ya kuhamia Dodoma inafanyika kidigitali  badala ya kuhama na maroli ya maboksi ya makaratasi.

Jaji mkuu ametoa kauli hiyo jijini Dodoma, wakati akifungua Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Mahakama ya Tanzania. Amesema safari ya kuhamia Dodoma ni lazima ifanyike kidigitali na sio kianalogia, maboresho sio majengo tu na mifumo ya tehema pia

Amesema watumiaji wa Mahakama na wananchi wanategemea kila mtumishi wa Mahakama aonyeshe na kudhihirisha kuwa Maboresho hayaishii katika kukamilisha majengo ya kisasa yaliyounganishwa na mifumo ya kisasa ya teknolojia.  

Wananchi na watumiaji huduma za Mahakama wanataka utamaduni mpya wa utoaji haki uliotokana na hayo maboresho ya mahakama. Ubora wa Majengo unapimwa kwa ubora wa huduma inayopatikana kutoka katika majengo

Ametumia Baraza hilo kuendelea kuwakumbusha kuwa utoaji wa huduma kwa umma katika Karne ya 21 ni tofauti kabisa na ilivyokuwa miaka michache tu iliyopita.  Hivi karibuni, tumeona juhudi kubwa za Serikali ya Tanzania kuongeza matumizi ya TEHAMA katika karibu kila nyanja ya utoaji wa huduma za umma.  

Amesema, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inatekeleza Mpango wa Dijitali Tanzania (Digital Tanzania Project) na kutaja malengo ya Mradi huo kuwa ni kuongeza upatikanaji wa huduma za umma kwa urahisi, ubora, uwazi, ufanisi na kwa bei nafuu.

 

 

 

Post a Comment

0 Comments