MBUNGE ASHAURI WIZARA YA ELIMU ICHANGANYE LUGHA KATIKA UFUNDISHAJI

 ðŸ“ŒRHODA SIMBA

SERIKALI kupitia Wizara ya Elimu imeshauriwa kuchanganya lugha mbili   katika ufundishaji ambazo ni lugha za kiuchumi na lugha ya Ufaulu ili taifa liweze kusonga mbele.

Akizungumza wakati akichangia makadirio ya  mapato na matumizi ya  bajeti ya Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia  Mbunge wa Jimbo la Pangawe  Zanzibar  Haji Amri Haji amesema kuwa nchi nyingi za ulaya zilizoendelea zimekuwa zikitumia lugha zao kwa sababu ya  mfumo wa kibiashara na mfumo wa kiuchumi na imewafanya kukua kimafanikio.

Ninachotaka kumanisha ni kwamba kwa sisi Tanzania   tunapaswa kubadilika katika ufundishaji wa lugha tunapaswa kuchanganya lugha mbili  ya kiuchumi na lugha ya ufaulu  ambapo katika ufaulu mtu anaweza kujifunza lugha kwa namna  yoyote

Mimi binafsi nina mawazo kwamba ili nchi iweze kuendelea tunapaswa kuwa na lugha mama ya kiswahili na kama tunataka lugha ya ufaulu tungechanganya lucha zote sio kiingereza tu hata kifaransa na lugha nyunginezo

Haji.

 

 

Post a Comment

0 Comments