NAIBU WAZIRI KUWAINUA KIUCHUMI WAJASIRIAMALI WADOGO

 ðŸ“ŒWILSON JOHN

NAIBU Waziri wa kilimo Mhe.Antony Mavunde amewatoa hofu wajasiriamali jijini Dodoma ikiwemo kuwawezesha kiuchumi pamoja na kuanzisha Tuzo ya MAVUNDE yenye lengo la kuwapatia milioni ishirini kwaajili ya kununua mashine itakayosaidia kuongeza uchakataji katika viwanda

Ameyasema hayo leo Mei 30, Jijini Dodoma wakati akifunga Mafunzo ya zunguka na mama program yenye lengo la kuinua uchumi wa wafanyabiashara wadogowadogo na uchumi wa viwanda  (WAUVI)

Mh. Mavunde amesema wajasiriamali wanatakiwa kutengeneza vikundi vitakavyowasaidia kuweza kupata mikopo ili waweze kujiinua kiuchumi na kuinua kipato cha mtu mmoja mmoja pamoja na taifa kwa ujumla

Niwaombe wajasiriamali kufanya uteuzi nipate watu kumi kwaajili ya kuwapeleka maonesho ya sabasaba nauli nitatoa mimi nataka nifanye hivi kwa ajili ya kuwapatia mafunzo yatakayosaidia kuinua na kubadilisha biashara zenu

Naye Mkurugenzi wa Shirika la Viwanda na wanawake kiuchumi Bi. Abiba Saidi amewataka wanawake kuchangamkia fursa na kusaidiana na waume zao katika kulea familia kwa ajili ya kupunguza majukumu ya kutunza familia. Lakini pia amewataka wajasiriamali kufanya kazi kwa vitendo ili kuweza kuingia katika soko la ushindani

Naiomba Serikali kupitia ofisi yako Naibu Waziri wa kilimo Mh.Mavunde kuna bidhaa nyingi zinazalishwa na wajasiriamali wetu lakini changamoto kubwa ni ukosefu wa nembo ya ubora TBS, naomba wajasiriamali wapatiwe nembo ya tbs ili waweze kuingia katika soko la ushindani

 

 

 

Post a Comment

0 Comments