SERIKALI IJE NA NJIA YA MAGONJWA YASIYO YA KUAMBUKIZWA KUTIBIWA BILA MALIPO "MBUNGE AIDA"

 ðŸ“ŒSAIDA ISSA

KUPITIA Bajeti ya Wizara ya Afya kwa mwaka wa fedha 2023/2024 Mbunge wa Nkasi Kaskazini Aida Khenani ameiomba Serikali kuja na njia mbadala ya kusaidia kwa magonjwa yasiyo ya kuambukiza kutibiwa bila malipo.

Mbunge huyo ameyasema hayo katika viwanja vya Bunge ambapo amesema kuwa ipo haja ya serikali kuingilia kati na kulitizima jambo hilo kwa kuhakikisha magonjwa hayo yasiyo ya kuambukiza kuhakikisha matibabu yake yanakuwa bure.

Mbunge Aida amesema kuwa Serikali ikiondoa Kodi ya matibabu katika magonjwa yasiyo ya kuambukiza kama vile kisukari, Kansa, kifafa pamoja na ajari itasaidia kuokoa maisha ya watanzania wengi.

Amesema kuwa kwa magonjwa yasiyo ya kuambukiza gharama ni kubwa na ngumu kwa mtanzania wa kawaida kuweza kumudu kulipa matibabu hayo.

Yapo magonjwa ambayo yanaweza kumtokea mtu yoyote mfano ajali inaweza kukukumba hata ukiwa nyumbani inaweza kupata ajali, suala la ajali ni lazima Serikali ilitazame kwa kina na namna ya kuweza kuwasaidia watanzania


 

Post a Comment

0 Comments