WADAU WA ELIMU JIJINI DODOMA WAMETOA PONGEZI KWA WIZARA

 ðŸ“ŒAMISA AMIRI & WILSON JOHN

WAKAZI wa Jiji la Dodoma wameiomba Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia  kukamilisha mapitio ya Sera ya elimu na mafunzo ya mwaka 2014 ikiwemo mitaala ya elimu na kuanza utekelezaji.

Wakitoa maoni yao jana Jijini hapa mara baada ya bajeti ya  Wizara ya  Elimu, Sayansi na Teknolojia kuwasilishwa bungeni na Waziri wa Wizara hiyo, Prof Adolf Mkenda wananchi hao wamesema mapitio ya sera hiyo yatasaidia  watoto kuongezeka shuleni na kutatua changamoto ambazo zinawakabili wanafunzi kielimu.

Mwalimu wa shule ya Sekondari Meriwa, Shukrani Nollo, amesema kutokana na serikali kuonekana ipo makini na Sera hiyo ya elimu imepelekea wao kama walimu kuheshimu nidhamu ya shule ambapo zamani walimu walikuwa wakitoka muda wowote  wanapojisikia kuondoka bila kutimiza majukumu wanayo takiwa ambapo imekuwa tofauti na sasa

Uboreshaji wa elimu kwa sasa kuna mabadiliko makubwa, kwanza elimu bure vijana wengi wamehamasika kusoma hata wazazi kwenye vikao wamekua wakijitokeza kwa wingi kutokana na kufatilia watoto wao

Kuboresha vifaa  kwa ajili ya mafunzo kwa vitendo zaidi hii itasaidia wanapo hitimu masomo yao waweze kujiajiri  kiurahisi pia kuongezeka kwa mshahara, tumeona Mei mosi sisi walimu serikali imetufikiria katika kuongeza mshahara hii inahamasisha ufundishaji

Nollo

Kwa upande wake Mwanafunzi wa Chuo Cha biashara (CBE) kampasi ya Dodoma Stera Benedict amesema uboreshaji wa elimu unaoendelea utawasaidia katika kuwatatulia changamoto ambazo wanakumbana nazo ikiwemo kupewa mikopo kwa ajili ya kujilipia ada na  kutengeneza miundombinu ambayo bado inaitaji marekebisho chuoni hapo

Amesema kwa wanafunzi wenye mahitaji maalumu kuweza kusaidia na kuboresha mazingira ya kujifunzia ikiwemo kufundishwa kwa vitendo ili kusaidia kupata uelewa mpana

Nashukuru kwa fursa ya mikopo kwani itasaidia sana kuweza kutatua changamoto za ada lakini pia kutupatia elimu itakayotuwezesha kupata ajira kwani hatuwezi kujiajiri wenyewe

Kuboresha miundombinu katika vyuo itasaidia kupunguza usumbufu, utakuta wanafunzi wengine wapo darasani halafu wengine wanahitaji darasa hii inapelekea  changamoto" Benedictor amesema

Katika mwaka wa Fedha 2023/2024 Waziri wa Elimu Adolf Mkenda amesema Wizara itakarabati maktaba na miundombinu mashuleni pamoja na majengo ili kuweka mazingira mazuri ya kujifunza kwa wanafunzi.

 

Post a Comment

0 Comments