WANAFUNZI VYUO VIKUU ACHENI VITENDO VYA RUSHWA YA NGONO

 ðŸ“ŒJASMINE SHAMWEPU

WANAFUNZI wa Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOM) wametakiwa kuacha na vitendo vya Rushwa ya ngono na kutaka kufaulishwa Katika masomo yao na badala yake wahakikishe wanakuwa mstari wa mbele kupinga na kuzuia vitendo vya Rushwa ya ngono.

Hayo yamesemwa na  rais wa Ndaki ya Sayansi Asilia na Hisabati Prof. Said Vuai wakati akifungua Warsha ya utoaji wa Elimu juu ya kupinga  vitendo vya Rushwa ya ngono  pamoja na Elimu ya jinsia.

Warsha hiyo imewajumuisha wanafunzi pamoja na wahadhiri wa Chuo hicho  iliyofanyika Jijini Dodoma

Rais huyo amewataka walimu waachane na vitendo vya Rushwa kwa kuwarubuni wanafunzi kwa kuwapa msaada wa kuwafaulisha mitihani yao.

Hakuna maendeleo  yoyote bila ya haki na haki haiwezi kupatikana kama kuna Rushwa hivyo kama kijana  umefaulu kwa njia ya Rushwa basi hata katika maeneo ya kazi utakayoenda yatakuwa na changamoto na kusababisha Rushwa

Rais .

Kwa upande wake mtoa mada kutoka  Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Dodoma Faustine Malecha amesema kuwa zipo tabia ambazo zinapelekea Rushwa ambapo ameitaja mojawapo ni pamoja na  kuiga vitu ambavyo sio desturi ya watu wa Kitanzania vinapelekea vijana hawa kujikita katika Rushwa .

Zipo aina nyingi za rushwa ila Rushwa ya ngono katika Elimu ya juu imekithiri hivyo niwatake vijana acheni kutumia Rushwa ya ngono kwa kuhisi mtafanikisha maisha kwa haraka

Malecha

Naye Daktari Bingwa wa Magonjwa ya kina mama na uzazi Dk Gabriel Kitunusa amesema kuwa wanafunzi wengi wanapata Elimu zisizo rasmi huko mitaani kuhusiana na mambo ya jinsia na mambo ya uzazi na kupelekea kupata changamoto za kutoa mimba na kusababisha vifo.

Pia amesema changamoto kubwa ambazo wanafunzi hawa wanakutana nazo ni kupata mimba zisizotarajiwa na wengine kupata maambukizi ya VVU pamoja na Magonjwa ya zinaa ambapo amewataka waachane na Elimu ya mitaani  na mienendo mibovu ya kimaadili.

Ikumbukwe kuwa Ndaki ya Sayansi Asilia ya Hisabati ina jukumu la kufundisha,  kufanya utafiti kutoa huduma kwa jamii kupitia  utaalamu wa utafiti pamoja na malengo mengine yanayohusiana na Rushwa na maswala ya Afya ya Uzazi.

 

 

Post a Comment

0 Comments