WANAUME WATAKIWA KUWA VINARA WA KUPINGA MIMBA NA NDOA ZA UTOTONI NCHINI.

 ðŸ“ŒJASMINE SHAMWEPU

WANAUME wameombwa kuacha kujihusisha kimapenzi na watoto walio chini ya miaka 18 na badala yake wametakiwa kuwa vinara katika kuhakikisha kwamba wanapinga vikali mimba na ndoa za utotoni Nchini

Fatuma Tawfiq Mbunge wa Viti Maalumu na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu  ya Bunge ya ustawi na Maendeleo ya jamii ameyasema hayo jijini Dodoma walipokuwa wamekutana na Kamati ya  Utawala Katiba na Sheria na Mtandao wa kupinga ndoa na mimba za utotoni  huku wakiangalia na kuijadili sheria ya ndoa ya mwaka 1971.

Mbunge huyo wa Viti Maalumu amesema  ndoa na mimba za utotoni haziwezi kukoma ikiwa wanaume hawataacha tabia zao za kutembea na mabinti wenye umri mdogo.

Rai yangu kama mzazi na kiongozi jambo hilo linatakiwa kubebwa na wanaume kwani watoto hawa wamekuwa wakipewa  mimba na  wanaume tena watu wazima ni mara chache sana unakuta mtoto kapewa mimba na mtoto mwenzake lakini asilimia kubwa wanaowapa mimba mabinti zetu ni hawa wanaume watu wazima sasa ni wakati wa kubadilika

Kama ninyi wanaume mtasimama na kuhakikisha mnalipinga suala hili basi tatizo la ndoa na mimba za utotoni  litakuwa limekwisha ndani ya nchi yetu

Mbunge Tawfiq.

Aidha amesema mjadala huo umekuja baada ya kesi ya mwanaharakati Rabeca Gyumi baada ya kuishitaki Serikali juu ya sheria ya ndoa kwani vifungu vya sheria vya ndoa vina makosa kwani katiba inasema mtu mzima ni mwenye umri wa kuanzia miaka 18 lakini  kisheria inasema mtu anaweze kuolewa akiwa na umri wa miaka 14 hadi 15 kwa umri wa Mahakama.

Amebainisha kuwa katika kesi hiyo ya mwanaharakati huyo mahakama ilitoa hukumu na katika kesi ile Serikali ilishindwa kesi.

Hapa nchini kuna watu wanaimani, dini, mila na desturi tofauti Serikali iliona jambo hili lipelekwe katika jamii ili kupata maoni na kuona ni namna gani bora ya kwenda na hiyo Sheria ili kila mtu asione ameumizwa, kukandamizwa au kuingiliwa katika imani, mila na desturi zao

Amesema ushauri wao kama bunge elimu itolewe katika jamii kwani Sheria hiyo itapelekwa bungeni lakini ukweli ni kwamba bado elimu inatakiwa itolewe katika jamii na katika elimu tunatumbua wazi Sheria ya elimu inayowataka watoto wote waende shule hivyo kwa hali hiyo tutakuwa tumewalinda moja kwa moja,  tutakuwa tumewalinda watoto kwa ndoa na mimba za utotoni.

Sesilia Bosco Mkuu wa Idara wa Mawasiliano na uchechemuzi shirika la Plan international amesema changamoto ya mimba za utotoni bado ipo kwa ukubwa sana katika mikoa ya Tanzania ambapo mikoa inayoongoza ni pamoja na mkoa wa Shinyanga kwani takwimu inaonyesha ipo juu sana licha kwa baadhi ya mikoa imekuwa ikishuka na kupanda. 

Amesema kutokana na hali hiyo wameshirikiana na Mtandao wa kutokomeza mimba za utotoni Tanzania na wabunge Kamati ya katiba na Kamati ya Maendeleo ya jamii kwani wana imani kipindi hiki ndio kipindi sahihi kwa wabunge kuweza kurekebisha sheria  ya ndoa ya mwaka 1971 kwani imekuwa ikimkandamiza mtoto  kwa kumruhusu mtoto wa kike kuolewa akiwa na umri wa Miaka 14.

Jitihada hizo zilianza muda mrefu lakini hakuna mabadiliko yoyote, mwaka jana ndio tuliona mabadiliko kidogo kwani tuliona utaratibu wa kuweza kubadilisha sheria hiyo na tuliona hatua za kukusanya maoni kwa wadau zilionekana

 

Post a Comment

0 Comments