WAZAZI NA WALEZI SIMAMIENI MAADILI KWENYE FAMILIA ZENU-GWAJIMA

 ðŸ“ŒAMISA AMIRI

WAZIRI wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu Dk.Dorothy Gwajima amewataka wazazi na walezi kusimamia malezi ya watoto wao kikamilifu ili kulinda Maadili kwa watoto na Jamii nzima.

Dk. Gwajima amesema hayo Mei, 15,2023,jijini Dodoma katika maadhimisho ya kitaifa ya familia  yaliyofanyika katika viwanja vya Nyerere square, na kusema kuwa suala la Maadili  katika Jamii ya sasa yamekuwa   tofauti na zamani  ambapo wazazi walikuwa  wakiwakusanya watoto wao  na kuwaelekeza namna bora ya kuishi na Jamii inayowazunguka.

Amesema kuwa Maadili yanayohitajika katika Jamii ni Maadili yanayoanzia katika familia kwa kuhakikisha kila mzazi anamrithisha mtoto Maadili bora ili kujenga taifa bora la leo na kesho. Pia amesema kupiga na kuuwa  kwa mzazi sio suruhisho tosha la mgogoro kwa watoto  hivyo ni bora kila mzazi kuhakikisha anapata muda wa kukaa na kuangalia Maadili ya watoto wake ndani ya familia kwa kufanya mazungumzo na kutatua changamoto zinazo wakabili watoto.

Tulinde sana watoto kuliko kitu chochote ili tuimarishe familia bora katika ustawi mzuri wa familia na taifa kwa ujumla na kupigania Maadili ya Jamii mzima. Maadili yakiwa mazuri hatutakuwa na tatizo lolote na hatutakuwa na mabadiliko ya kijamii kuhusu vitendo vinavyotokea hapa matukio haya ni kukosekana kwa Maadili ndani ya Jamii yetu.

Maadili sio kitu kidogo kwa watoto, wazazi tuwape maadili, malezi na mafunzo bora  watoto itakuwa ni bora sana kwao kuliko kumpa zawadi. Ukimpa mtoto Malezi Bora yatamsaidia sana kuliko vitu vimpatia upendo wa siku moja, kwahiyo inabidi tuangalie sisi kama wazazi na walezi ni kitu gani watoto wetu wanastahiki ndani ya Jamii yetu..

Dk.Gwajima

Aidha Mbunge wa Dodoma Mjini Mh. Antony Mavunde  amesema katika mkoa wa Dodoma kulikuwa na changamoto ya watoto wengi wa mitaani jambo ambalo linatokana na kutelekezwa kwa watoto ndani ya familia na kukosa malezi bora ya familia hivyo kuwaomba wazazi kuwa na upendo na watoto wao.

Amesema kutokana na kuwa na watoto wengi wa mitaani  inaonyesha kuwa wazazi hawapo makini kuwalea watoto wao kikamilifu kama inavyopaswa na sababu kubwa ambayo walikuwa wakiitaja watoto hao wanaoishi mitaani ni wazazi kutokutimiza majukumu yao .

Sasa basi tuwe makini kulinda na kuwapa Maadili wa watoto, viongozi, wazazi lakini pia machifu tusaidizane katika suala la Maadili huko kwenye maeneo yetu tutakuwa na watoto wema

Sisi kama wazazi lazima tuwe tayari kuhakikisha tunalinda watoto wetu na kutowanyanyapaa ili tu tuepukane na matendo tunayoyasikia niombe tu viongozi wa dini, machifu ili tuangamize haya mambo mengine tunayoyasikia ndani ya Jamii yetu

Naye aliyekuwa Waziri wa Katiba na Sheria, Prof. Palamagamba Kabudi, amewahimiza viongozi wa dini kutoa elimu ya dini katika kujenga Maadili katika Jamii jambo ambalo litawasaidia watoto kuwa na makuzi na Maadili ya Mungu katika maisha yao.

Viongozi wa dini tunawaomba muwe kipaumbele na tunawategemea sana katika suala la kuwapatia elimu ya dini ikiwemo na Maadili huko kwenye maeneo yenu nadhani nyie mtatusaidia katika hilo.

Elimu tunayoitaka kwa watoto wetu tukiipata basi Jamii tutakuwa tumeipeleka sehemu stahiki pia wewe kama mzazi kamili ni lazima kuhakikisha familia hasa watoto kujua Maadili yao ndani ya familia .

 Kabudi

Pia Dk.Gwajima amesema Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Samia Suluhu Hassan amejitoa kwa kujenga madarasa ili kukabiliana na ongezeko watoto wa mitaani.

 

 

 

Post a Comment

0 Comments