ZINGATIENI UKWELI, UWIANO, USALAMA NA MAADILI YA UANDISHI WA HABARI

Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Dodoma akisisitiza jambo wakati wa Maadhimisho ya Uhuru wa vyombo vya Habari jana (21/05/2023) yaliyofanyika kimkoa katika Ukumbi wa Roma Complex

📌WILSON JOHN &  AMISA AMIRI.

MWENYEKITI wa Klabu  ya Wandishi wa Habari Mkoa wa Dodoma Bw. Musa Yusufu   amewataka  Wandishi wa habari jijini hapo, kujithamini na kujitambua  katika taaluma ya Uandishi na  Utangazaji lakini pia kupendana na kupatana wanapotofautiana miongoni mwao na sio kutupiana vijembe wala kujenga chuki baina yao.

Kauli hiyo ameitoa wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya habari Duniani ambayo Kimkoa (Dodoma ) yamefanyika tarehe 21 Mei, 2023 katika Ukumbi wa Roma complex ambapo wanahabari wanachama wa Klabu walifanya Mdahalo katika kuchagiza kauli mbiu ya mwaka 2023 ambayo inasema “Kuunda mustakabali wa Haki, Uhuru wa kujieleza kama kichocheo cha Haki nyingine za binadamu”

Bw. Musa Yusufu amesema tabia ya kununiana na kuchukiana inajenga taswira mbaya katika jamii kwa Wandishi wa habari na kushusha thamani ya Wandishi wa habari

Wandishi tupendane na kuheshimiana miongoni mwetu,  maana kuna watu wananuniana na kutupiana vijembe, sasa haya mambo yaishe leo tuzungumze pamoja na kushirikiana katika kazi

Niwaombe ndugu wandishi kila mmoja afanye kazi yake, kuna tabia imejitokeza sio nzuri na inatushushia heshima. Suaala la kwenda kwenye mkutano hujaalikwa baadae unataka usaini ili upate pesa si jambo zuri. Kama hujaalikwa nenda kachukue habari kisha waachie wahusika mambo mengine 

Yusufu 

Kwa upande wake mjumbe na mwaandishi wa habari Mkongwe Joyce Kasiki amesema nidhamu  kwa wandishi wa habari imeshuka kadri siku zinavyozidi kwenda. Amesema baadhi ya wandishi wa habari wamekua na tabia mbaya kiasi cha kushusha heshima kwa tasnia ya Uandishi wa habari kutokana na tabia zisizofaa miongoni mwao.

Niwazungumzie Wandishi wapya, wakati sisi tunaanza kazi suala la kuhudhuria mikutano na kupata fedha tulikua tunalisikia kwa mabosi wetu lakini sasa mtu anaanza kazi leo kesho kuna mkutano Morena na pesa anachukua, sasa mtu huyu hawezi kufanya kazi kwa weledi

Nasikitika kusikia kuwa kuna watu wana zaidi ya vyombo vinne hadi vitano linapofika suala la kusaini mtu anajitokeza na  kasema fulani kasema nimchukulie hii, inashusha thamani kwa Wandishi wa Habari tubadilike

Joyce 

Hata hivyo Okuly Julius amesema baadhi ya Wandishi wa Habari wamekua wakivaa mavazi ambayo hayafai na kuleta tofauti kiasi cha kujulikana na kuzungumziwa tofauti kitu kinacholeta taswira mbaya kwa wadau na jamii kwa ujumla

Kuna wandishi jinsi wanavyovaa na mwandishi huyo huyo anahitaji kupata story jambo ambalo watu wamekua wakitushangaa na kutuzungumzia hawa ni wandishi? Kwa  jinsi tunavyovaa

Kwa upande wa maslahi Okuly amesema

Imefikia wakati watu Sasa tunatishiana kisa mtu hajapata fedha, kwenye mkutano hujaalikwa halafu unataka usaini, mtu huyuhuyu ukionesha kumkatalia anaanza kukutishia hebu tuache hayo mambo tufanye kazi

Okuly

Makamu Mwenyekiti wa Klabu ya Wandishi wa habari Karate Mbashiru amewataka Wandishi wa habari kuheshimiana na kujitambua na kusema ukiwa mwaandishi moja punguza ujuaji, kubali kujifunza na kukosolewa.

Maadhiisho ya Uhuru wa vyombo vya habari duniani hufanyika kila mwaka ifikapo tarehe 3 Mei.

                                       




Post a Comment

0 Comments