VIJANA WAENDESHA MAISHA YAO KUPITIA KAZI YA MATAIRI


📌AMISA AMIRI.

VIJANA kutoka Mtaa wa  Bahi Road jijini Dodoma wameweza kujiajiri katika kazi ya kutengeneza bidhaa zitokanazo na matairi mabovu ya magari, iliyowasaidia kuboresha maisha yao  na kukuza uchumi wa taifa  kupitia kutengeneza bidhaa tofauti tofauti .

Mwenyewekiti Silivester Comando ambaye ni kingozi wa kusimamia vijana hao wanaofanya kazi ya kutengeneza bidhaa hizo ikiwemo viatu, Bush kwaajili ya magari na mipira ya kufungia mizigo amewataka vijana kuja kujiunga na kazi hiyo ili kuondokana na ongezeko la vijana wasio na ajira. 

Ameyasema hayo leo jijini humo wakati akizungumza na CPC Blog ambapo amesema kazi hii sio kazi ngumu inahitaji nguvu ya mikono na ujuzi kwaajili ya kutengeneza bidhaa hizo zinazowapatia ajira pia amesema nafasi zipo za kufanya kazi katika sehemu hiyo kwa vijana wasio na ajira mitaani.

Kwa vijana wasio na ajira wanakuja hapa wanapitia kwenye uongozi wa hapa tunawapa maelezo ya kuishi na sisi wanaanza kufanya kazi na hii kazi unaweza kuja asubuhi ukafanya kazi ukaondoka na zaidi ya shilingi 20,000/= kwa kiasi cha chini muda mwingine unaweza kupata hata laki moja kwa siku inategemea na siku yenyewe ipoje na wateja wako.

Lakini tumekuwa tukipata changamoto ya ajali za kujikata kwasababu tunatumia visu kukatia mataili pia kuna  changamoto ya eneo la kufanyia kazi kuwa dogo 

 Comando.

Kwa upande wake Baraka Tonny amesema kwasasa ana miaka zaidi ya saba katika kufanya kazi hiyo na imeweza kumnufaisha  kimaisha ambapo amejenga nyumba na kuweza kupata familia kwa kipindi ambacho amekuwa akijishughulisha na kazi hiyo hadi sasa.

Malighafi hizi tunazipata kwa madereva wanaoendesha gari kutoka sehemu mbalimbali  huko mikoani na kila tairi lina gharama yake inategemea na ukubwa wa tairi kwasababu kuna tairi kubwa na dogo.

Natengeneza bush za magari na mipira ya kufungia mizigo bei ni ya kawaida sana kuazia elfu mbili na kuendelea. Kwa siku naweza kuuza kuazia elfu 30,000/= mpaka laki moja na elfu sitini (160,000/=)

Tonny.

Hata hivyo mwisho mwenyekiti amewatoa wasiwasi wateja wanaokuja kununua bidhaa katika eneo hilo kwa tetesi za kuhamishwa kutoka walipo kwenda sehemu nyingine amesema kuwa sio kweli na kama itatokea basi watafata utaratibu unaotakiwa ila kwasasa wapo katika eneo hilo  na wanaendelea kufanya kazi .


Post a Comment

0 Comments